Tumaini Kuu
Mungu Mke wa Hekima
“Kusimikwa kwa mungu mke wa hekima kulikuwa kunarudiwa rudiwa na kufuatishwa katika taifa zima, na kwenye maeneo ambayo wenyeji wake walikuwa wanatamani kwenda pamoja na Mapinduzi.” 175 TK 178.3
Alipoletwa kwenye mkutano, msemaji aliushika mkono wake na kuugeukia mkutano na kusema: “‘Ninyi watu, acheni kutetemeka mbele ya ngurumo zisizokuwa na nguvu za Mungu ambaye kwa hofu yenu mnadhani kuwa yupo. Tangu sasa na kuendelea, msimtambue Mungu ye yote isipokuwa mungu mke wa hekima. Ninawapatieni sanamu yake nzuri na safi isiyolinganishwa na chochote, na endapo mtalazimika kuwa na sanamu nyingine, toeni kafara kwenye sanamu hii peke yake.... TK 178.4
Baada ya kukumbatiwa na mwenyekiti mungu mke alipakizwa kwenye gari la fahari na kupelekwa kwenye kanisa la dayosisi kule Notre Dame, na kuchukua nafasi ya Mungu. Na hapo mungu huyu aliwekwa juu ya mimbari iliyokuwa imeinuliwa sana na watu wote waliokuwa pale wakamwabudu.” 176 TK 178.5
Utawala wa Papa ulianzisha kazi ambayo ukanamungu ulikuwa unaikamilisha, na kuiharakisha nchi ya Ufaransa kuelekea kwenye maangamizi. Wakirejea vitisho vya Mapinduzi, waandishi wanasema, mambo haya yaliyokithiri yalikuwa yanatakiwa kubebeshwa kwenye kiti cha enzi cha kanisa.(Angalia Kiambatisho) Na kwa hali halisi ni sharti lawama juu ya jambo hili ziende kwa kanisa. TK 179.1
Utawala wa Papa ulikuwa umesumisha vichwa vya wafalme dhidi ya imani ya Matengenezo Nguvu za Roma zilikuwa zimeweka msukumo wa ukatili na ukandamizaji uliokuwa unatoka katika kiti cha enzi. TK 179.2
Popote Injili ilipopokelewa, mioyo ya watu ilizinduliwa. Wakaanza kuitupilia mbali minyororo iliyokuwa imewafunga kwenye utumwa wa ujinga na imani za kishirikina. Wafalme waliishuhudia na kutetemeka kwa sababu ya utawala wao wa kidhalimu. Utawala wa Papa ulifanya haraka kuchochea hofu yenye wivu ya wafalme hawa. TK 179.3
Mnamo mwaka 1525 Papa alisema maneno yafuatayo kwa mtawala wa Ufaransa: “Wazimu huu [yaani Uprotestanti] hautachanganya na kuharibu tu mambo ya dini bali mamlaka zote, tabia njema, sheria na mpangilio wa maisha ya watu.” TK 179.4
Balozi wa Papa alimwonya mfalme kwa maneno haya: “Waprotestanti watavuruga utaratibu wote wa kiraia na ule wa kidini....Kiti cha enzi cha mfalme kiko hatarini kama vile mimbari ilivyo hatarini.” 177 Kanisa la Roma lilifanikiwa kulipanga taifa la Ufaransa tayari kupiga vita imani ya Matengenezo. TK 179.5
Mafundisho ya Biblia yangejenga ndani ya mioyo ya watu kanuni za haki, kuwa na kiasi, ukweli, mambo ambayo ni mhimili wa ustawi wa taifa. “Haki huinua taifa.” Na kwa namna hiyo “kiti cha enzi huthibitishwa.” Mithali 14:34; Isaya 16:12 (Soma Isaya 32:17.) Anayetii sheria ya Mungu pia ataheshimu na kutii sheria za nchi. Ufaransa ilipiga marufuku Biblia. Watu waaminifu na wenye nguvu kiakili na kimaadili, waliokuwa na imani kuvumilia mateso kwa sababu ya ukweli walipata taabu kubwa, baharini waliangamia kwenye nguzo ya kuchomea moto “waasi” ama waliachwa kuoza katika magereza yaliyokuwa chini ya ardhi. Maelfu walikimbilia mahali pa usalama miaka 250 baada ya imani ya Matengenezo kuanza. TK 179.6
“Kwa nadra kulikuwa na kizazi cha Wafaransa kwenye kipindi hiki kirefu ambacho hakikushuhudia wafuasi wa Injili wakikimbia mateso makali, wakichukua pamoja nao ujuzi, ustadi, uchapa kazi, mfumo wa maisha, ambapo kama kanuni ilivyo, walikuwa wamefanikiwa sana, hivyo kuzinufaisha nchi zilizokuwa zimewapatia hifadhi.... Endapo watu wote waliokuwa wamefukuzwa wangebaki nchini Ufaransa ...taifa hili lingekuwaje...taifa kubwa, lenye ustawi, na nchi yenye kuvutia- ingekuwa kielelezo kwa mataifa mengine! TK 180.1
Lakini ufinyu wa kuelewa na kutochukuliana na watu wenye mtazamo tofauti uliwafukuza kutoka kwenye ardhi yake kila mwalimu mwadilifu, kila mtetezi wa mfumo safi wa maisha, na kila mlinzi wa kiti cha enzi cha ufalme wa nchi hiyo...Hatimaye uangamivu wa taifa ulitimia.” 178 Matokeo yake yalikuwa ni Mapinduzi ya kuogofya. TK 180.2