Tumaini Kuu

93/254

Ushupavu katika Kumtukana Mungu

Mmoja wa mapadre wa shirika jipya alisema, “Kama wewe Mungu upo, jilipizie kisasi kwa sababu jina lako linatukanwa. Ninakudharau! Unabaki kimya; Huthubutu kuzituma ngurumo zako. Ni nani baada ya jambo hili atakayeamini kwamba Upo?” 174 Maneno haya yanaakisi kiasi gani yale madai ya Farao! kwamba: “BWANA ni nani hata niweze kuitii sauti yake?” TK 177.4

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Na Bwana anasema “...Maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote.” Zaburi 14:1, 2; 2 Timotheo 3:9. Baada ya Ufaransa kukataa ibada ya Mungu aliye hai, nchi hiyo iliporomoka kuelekea kwenye ibada ya sanamu iliyokuwa duni sana kwa kuanza kumwabudu mungu mke wa Hekima (Goddess of Reason)- mwanamke mzinzi. Jambo hili lilifanyika kwenye Bunge la nchi hiyo! “Mojawapo ya sherehe za kiwendawazimu za wakati huu inayosimama bila mshindani kwa upumbavu unaojumuisha uovu. TK 178.1

Milango ya ukumbi wa mikutano ilifunguliwa... Wajumbe wa baraza la mji waliingia kwa maandamano mazito, wakiimba wimbo wa sifa kwa sababu ya uhuru wa kujiamulia mambo, walikuwa wanasindikiza kitu cha kuabudiwa katika siku za usoni, sanamu ya mwanamke iliyokuwa imefunikwa, waliyokuwa wanaiita mungu mke wa hekima. Ilipoletwa ndani ya ukumbi ilifunuliwa kwa mwonekano wa kuvutia na kuwekwa upande wa kuume wa mwenyekiti na alitambuliwa kuwa ni msichana achezaye muziki kwenye ukumbi wa maonesho.” TK 178.2