Tumaini Kuu

92/254

Uovu wa Kutisha zaidi

Jambo la kuogofya kati ya matendo ya kishetani ya kame za kutisha yalikuwa ni mauaji ya halaiki ya St. Bartholomew. Mfalme wa Ufaransa aliombwa kibali na mapadre na maaskofu. Kengele iliyongongwa usiku wa manane ilikuwa ni ishara ya mauaji. Wakiwa wamelala kwenye nyumba zao, wakitumaini kuwa mfalme wao atawastahi, Waprotestanti kwa maelfu walikokotwa toka huko na kwenda kuuawa. TK 176.1

Kwa muda wa siku saba mauaji yalikuwa yanaendelea mjini Paris. Kwa agizo la mfalme mauaji haya yalisambaa kwenda kwenye miji mingine walikokuwa Waprotestanti. Wakuu kwa wakulima, wazee kwa vijana, akinamama kwa watoto, waliuawa kwa pamoja. Waungwana wapatao 70,000 wa nchi yote ya Ufaransa waliangamia. TK 176.2

“Habari za mauaji hayo zilipofika Roma, mapadre walifurahia sana. Kardinali wa Lorraine alimzawadia mtu aliyepeleka ujumbe huo kwa taji elfu moja; Padre wa Kanisa Kuu la St. Angelo alibubujikwa na salamu za furaha; kengele ziligongwa kutoka katika kila mnara wa kengele wa kanisa; myoto mikubwa ya kusherehekea iligeuza usiku kuwa mchana; na Gregory XIII, alikuwa anawahudumia makardinali na wakuu wangine wa kanisa, walitembea katika msafara mrefu kwenye kanisa la St. Louis, mahali ambapo kardinali wa Lorraine aliimba wimbo unaosema Te Deum...Sahani ya chuma ilipigwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji hayo...Padre wa Kifaransa ...aliizungumzia siku hiyo kama siku yenye furaha tele na kuridhisha, wakati baba mtakatifu alipozipokea habari hizo alikwenda kwa umakini kumshukuru Mungu na Mtakatifu Louis.” 173 TK 176.3

Roho aliyeongoza mauaji ya halaiki ya St. Bartholomew ndiye aliyeongoza matukio ya Mapinduzi. Yesu Kristo alitangazwa laghai na sauti ya makafiri wa Ufaransa ilikuwa “Mponde Fidhuli,” kwa maana ya Kristo. Makufum na uovu vilikuwa vinakwenda bega kwa bega. Katika yote haya, Shetani ndiye aliyepewa heshima na utii, wakati Kristo katika tabia yake ya ukweli, usafi wa moyo, na upendo usiokuwa na ubinafsi, “alisulubiwa.” TK 176.4

“Mnyama atokaye kuzimu atafanya vita nao na atawashinda na kuwaua.” Ufunuo 11:7. Utawala usiomjua Mungu uliokuwa unatawala Ufaransa wakati wa Mapinduzi na Utawala wa Kidhalimu ulikuwa unafanya vita dhidi ya Mungu na Neno lake. Ibada ya Mungu ilipigwa marufuku na Bunge. Biblia zilikusanywa na kuchomwa moto hadharani. Taasisi za Biblia zilipigwa marufuku. Siku ya pumziko ya kila juma iliwekwa kando, na badala yake kila siku ya kumi ilitengwa kwa ajili ya sherehe na anasa. Ubatizo na Meza ya Bwana vilipigwa marufuku. Matangazo yaliyokuwa yamewekwa makaburini yalisema kuwa kifo ni usingizi wa milele. TK 177.1

Ibada zote za kidini zilipigwa marufuku, isipokuwa ile ya “uhuru wa watu kujiamulia mambo yao” na ya nchi. Askofu wa kikatiba wa mji wa Paris aliletwa mbele kutangaza kwenye Mkutano Mkuu kwamba ile dini aliyokuwa anaifundisha kwa miaka mingi ilikuwa ni sehemu ya maarifa ya mapadre, ambayo hayakuwa na msingi wowote kwenye historia au kwenye ukweli mtakatifu. Kwa maneno makini na ya wazi alikana uwepo wa Mungu ambaye kwa huyo aliwekwa wakfu kuhudumu ibada yake. TK 177.2

“Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa maana manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.” Ufunuo 11:10. Makafiri wa Ufaransa walinyamazisha sauti ya mashahidi wawili wa Mungu wanaoonya. Neno la Mungu lilikuwa limekufa na kulala kwenye mitaa yake. Na waliokuwa wanaichukia sheria ya Mungu walikuwa wanashangilia. Wanadamu walimdharau Mfalme wa mbinguni waziwazi. TK 177.3