Tumaini Kuu
Ladui Dhidi ya Kristo
“Hapo Bwana wetu aliposulubiwa.” Jambo hili pia lilitimia nchini Ufaransa. Hakuna nchi ambayo ukweli ulikumbana na upinzani mbaya sana kama hii. Mateso waliyokuwa wanafanyiwa waliopokea Injili nchini Ufaransa yalikuwa yanamsulubisha Yesu kupitia wafuasi wake. TK 175.1
Kame baada ya kame damu ya watakatifu ilikuwa inamwagika. Wakati watu wa kule Waldensia walipoyatoa maisha kwenye milima ya Piedmont “kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu,” ushuhuda kama wao ulikuwa unafanywa na watu walioitwa Albigenses wa Ufaransa. Wafuasi wa imani ya Matengenezo waliuawa baada ya mateso ya kuogofya. Wafalme, wakuu na mabinti zao, wanawali mahiri walikuwa wanajifurahisha kwa maumivu makali ya wafia dini Wakristo. Mashujaa wa jamii ya Huguenots walimwaga damu yao walipokuwa wanapambana, na walikuwa wanawindwa kama wanyama pori. TK 175.2
Wazao wachache wa Wakristo wa zamani waliokuwa wamebaki nchini Ufaransa kwenye kame ya kumi na nane, ambao walikuwa wamejificha milimani kusini mwa nchi hiyo, walikuwa wameihifadhi imani ya mababu zao. Walilazimishwa kwenda utumwani kwa vyombo vya baharini maisha yao yote. Watu waliofundishwa vizuri na wenye akili wa Ufaransa walikuwa katika mateso ya kutisha katikati ya wanyang’anyi na wauaji. Wengine waliuawa bila humma walipokuwa wanapiga magoti katika sala. Nchi yao ilikuwa imeharibiwa na upanga, shoka, moto, “ilikuwa imegeuzwa kuwa nyika kubwa yenye huzuni. TK 175.3
“Mauji haya ya kikatili yalifanyika...si katika zama za giza, lakini katika utawala wenye mafanikio wa Louis XIV. Kwa wakati huu sayansi ilikuzwa, elimu ilistawi, wakuu wa mahakama na ikulu walikuwa ni wasomi na wenye uwezo, na kwa kiasi kikubwa waliathiri neema ya unyenyekevu na upendo.” 172 TK 175.4