Tumaini Kuu

88/254

Upatanifu wa Sheria na Injili

Kwa wale waliokuwa wanadai kwamba “kuhubiriwa kwa Injili lilikuwa jibu la matakwa yote ya sheria,” Wesley alijibu: “Haijibu matarajio ya kwanza ya sheria, yanayoitwa, kuwathibitishia wanadamu kwa habari ya dhambi, na kuwaamsha wale wanaolala kwenye kingo za kuzimu...kwa hiyo ni jambo la kipumbavu kuwapatia daktari watu wenye afya njema, na hata wale wanaodhania kuwa ni wazima. Jambo la kwanza unatakiwa kuwathibitishia kuwa ni wagonjwa; vinginevyo hawatakushukuru kwa jitihada zako. Ni jambo la kipuuzi pia kumtoa Kristo kwa watu ambao mioyo yao ni mizima wala haijavunjika vunjika.” 169 TK 170.3

Kama alivyokuwa Bwana wake alipokuwa anahubiri Injili ya neema ya Mungu, Wesley “aliitukuza sheria na kuiadhimisha.” Isaya 42:21. Matokeo aliyoruhusiwa kuyaona yeye mwenyewe yalikuwa ni ya kupendeza sana. Wakati wa kuhitimisha huduma yake iliyozidi nusu kame, wafuasi wake walikuwa wamefikia idadi ya watu zaidi ya nusu milioni. Lakini kundi kubwa la watu lililonyanyuliwa kutoka kwenye hali duni ya maisha ya dhambi kwenda katika maisha safi na ya hali ya juu kutokana na juhudi zake kamwe halitajulikana mpaka familia yote ya waliokombolewa watakapokusanyika kwenye ufalme wa Mungu. Maisha yake yanatupatia fundisho la kima kisichopimika cha thamani ya maisha ya kila Mkristo. TK 171.1

Imani aliyokuwa nayo, kutochoka kwenye juhudi zake, kujitoa mhanga kwake, na utauwa wa mtumishi huyu Wakristo ungeweza kuakisiwa kwenye makanisa ya leo! TK 171.2