Tumaini Kuu

87/254

Kuilinda Sheria ya Mungu

Katika kujibu dai kuwa wakati Kristo alipokufa Amri Kumi za Mungu zilitanguliwa pamoja na sheria za kawaida za matendo ya dini, Wesley alisema, “Hakuiondoa sheria ya maadili iliyomo katika Amri Kumi iliyokuwa inashikwa na manabii. Hii ni sheria ambayo kamwe haiwezi kutanguliwa, ‘inasimama thabiti kama shahidi mwaminifu kule mbinguni.’ ” TK 169.3

Wesley alitangaza pia mapatano yaliyopo kati ya sheria ya Mungu na Injili. “Kwa upande mmoja sheria huendelea kutengeneza njia na kutuelekeza kwenye lnjili; na kwa upande wa pili habari njema huendelea kutuongoza kwa usahihi kuitimiza sheria. Mathalani sheria hututaka kumpenda Mungu, na majirani zetu; kuwa wapole, wanyenyekevu na watakatifu. Tunajisikia kwamba hatuna uwezo kuyatimiza haya;...lakini ahadi ya Mungu hutupatia upendo huo, na kutufanya kuwa wanyenyekevu, wapole na watakatifu: tunaing’ang’ania Injili na hizi habari njema...‘haki ya sheria inatimizwa ndani yetu,’ kwa njia ya imani iliyo katika Kristo Yesu.... TK 170.1

“Walio wakuu miongoni mwa maadui wa Injili ya Kristo,” asema Wesley, “ni wale wafundishao watu kuvunja, siyo amri moja tu, kati ya zile zilizo ndogo au zilizo kubwa, bali amri zote kwa mpigo. Wao humheshimu Mungu kama alivyofanya Yuda aliposema, ‘Salamu Rabi akambusu’.... Kuzungumzia damu yake, na kumvua taji yake; kuhafifisha sehemu yo yote ya sheria yake, kwa kisingizio cha kueneza Injili yake ni sawa na kumsaliti kwa busu.” 168 TK 170.2