Tumaini Kuu

22/254

Kushambuliwa na Ugonjwa wa Kutisha

Lakini kwa ghafla kazi zake zilisimimamishwa. Ingawa alikuwa hajafikia umri wa miaka sitini, kazi ngumu sana, majifunzo mengi na mashambulio ya maadui vilikuwa vimekula nguvu zake na kumfanya awe mzee kabla ya wakati wake. Alishambuliwa na ugonjwa wa hatari. Watawa walifikiri kuwa angetubu uovu aliokuwa amelifanyia kanisa, na wakaenda upesi kwenye chumba chake ili wasikie ungamo lake. “Mauti yamo midomoni mwako,” walisema, “guswa na makosa yako na tangua mbele yetu yote uliyoyasema na kutujeruhi.” TK 57.4

Mwanamatengenezo alisikiliza akiwa kimya. Kisha akamwomba mhudumu wake amuinue kitandani mwake. Huku akiwatazama kwa makini, alisema kwa uthabiti, kwa sauti yenye nguvu ambayo mara nyingi iliwatetemesha, “Sitakufa, nitaishi; na kwa mara nyingine nitayataja matendo maovu ya watawa.” 11 Wakiwa wameshangazwa na kutahayarishwa, watawa walikimbia kutoka kwenye chumba. TK 57.5

Wycliffe akaishi na kuweza kufikisha mikononi mwa watu wa nchi yake silaha iliyo kubwa kuliko zote dhidi ya Kanisa la Roma - Biblia, wakala aliyeteuliwa na mbingu ili kukomboa, kuelimisha na kuwafikishia watu Injili. Wycliffe alijua kuwa alikuwa amebakiza miaka michache tu ya kufanya kazi; aliona upinzani ambao ilipasa akabiliane nawo; lakini akiwa ametiwa moyo na ahadi za Neno la Mungu, aliendelea mbele. Huku akiwa na nguvu kamili zilizoonekana katika uwezo wake kiakili, uzoefu wa kutosha, kwa majaliwa ya Mungu aliandaliwa kwa ajili ya kazi hii iliyo kuu kuliko zote alizowahi kuzifanya. Mwanamatengenezo huyu akiwa katika nyumba yake ya Upadre kule Lutterworth, hali akiacha kufuatilia dhoruba iliyoongezeka nje, akazami kwenye kazi hii. TK 58.1

Hatimaye, kazi ilimalizika-tafsiri ya kwanza ya Biblia. Mikononi mwa watu wa Uingereza, mwanamatengenezo aliiweka nuru ambayo kamwe haingezimishwa. Alikuwa amefanya kazi kubwa zaidi katika kuvunja pingu za ujinga na kuikomboa na kuiinua nchi yake kuliko yote yaliyowahi kutekelezeka katika ushindi kwenye viwanja vya mapambano. TK 58.2

Nakala za Biblia zingeweza kuzidishwa tu kwa njia ya kazi ngumu chosha. Shauku ya kupata kitabu hiki ilikuwa kubwa kiasi ambacho watengenezaji wa nakala walipatagumu sana kufikia kiwango cha mahitaji. Wanunuzi waliokuwa matajiri walitaka Biblia nzima. Wengine walinunua sehemu tu. Mara nyingi, familia ziliungana na kununua nakala moja. Kwa muda mfupi, Biblia ya Wycliffe, kwa haraka ilifika majumbani mwa watu. TK 58.3

Wycliffe sasa alifundisha mafundisho yaliyowabainisha Waprotestanti wokovu kwa njia ya imani katika Kristo na kutokukosea kwa Maandiko. Imani hii mpya ilipokelewa na takriban nusu ya watu wa Uingereza. TK 58.4

Kuonekana kwa Maandiko kulileta fadhaa kwa mamlaka za kanisa. Wakati huu Uingereza haikuwa na sheria inayokataza Biblia, kwani ilikuwa haijawahi kuchapwa katika lugha ya watu. Sheria hizi zilipitishwa baadaye na kushinikizwa kwa ukali. TK 58.5

Kwa mara nyingine viongozi wa utawala wa Papa waliandaa mpango wa kuizima sauti ya Mwanamatengenezo. Kwanza, sinodi ya maaskofu ilitamka kuwa mafundishoyake yalikuwa ya kizushi. Baada ya kufaulu kumshawishi mfalme kijana, Richard II, walipata tamko la kifalme kuwa kila mtu ambaye angeshikilia mafundisho yaliyokatazwa apelekwe gerezani. TK 58.6

Wycliffe akapeleka rufani yake toka kwenye Sinodi hadi kwenye Bunge. Bila ya hofu alishitaki mamlaka ya Papa mbele za baraza la taifa na kudai badiliko la desturi mbaya sana za ukatili zilizoidhinishwa na kanisa. Adui zake wakapatwa na kiwewe. Ilitegemewa kuwa Mwanamatengenezo, wakati wa uzee wake, akiwa peke yake na bila marafiki, angejisalimisha kwa ufalme. Lakini badala yake, Bunge, likiwa limeamshwa na miito inayoshtua ya Wycliffe, liliondoa sheria, na Mwanamatengenezo akawa huru tena. TK 59.1

Kwa mara ya tatu aliletwa kwenye shitaka, na sasa ikiwa ni mbele ya Mahakama ya kikanisa katika ufalme. Hatimaye hapa kazi ya Mwanamatengenezo ingesimamishwa. Ndivyo wafuasi wa utawala wa Papa walivyodhani. Kama wangekamilisha kusudi lao, Wycliffe angetoka kwenye baraza hilo kuelekea kwenye miali ya moto na sio vinginevyo. TK 59.2