Tumaini Kuu
Kutoridhika Miongoni mwa Malaika
Akiiacha nafasi yake mbele ya uwepo wa Mungu, Lusifa alisonga mbele katika kueneza kutokuridhika kwake miongoni mwa malaika. Kwa mafumbo yenye usiri, akilificha kusudi lake halisi chini ya mwonekano wa uchaji wa Mungu, alijitahidi kuchochea kutoridhika juu ya sheria zilizoongoza viumbe wa mbinguni, akitangaza kwamba zililazimisha vizuizi visivyo vya lazima. Kwa vile malaika ni watakatifu, alitoa hoja kwamba wangepaswa kufuata matakwa ya nia zao. Mungu hakumtendea haki kwa kumpa Kristo mamlaka kuu. Alidai kwamba hakuwa akitafuta kujiinua nafsi bali kuwahakikishia uhuru wakazi wote wa mbinguni, ili waweze kupata maisha bora zaidi. TK 307.1
Mungu alimvumilia Lusifa kwa muda mrefu. Pamoja na kutoa madai potovu mbele za malaika, Mungu hakumshusha daraja kutoka katika nafasi yake iliyokuwa juu. Mara kwa mara alipewa msamaha kwa sharti la toba na kujisalimisha. Juhudi hizo, ni upendo usio na mwisho pekee ambaoungeweza kuzibuni, ili kumshawishi atambue kosa lake. Hali ya kutoridhika haikuwahi kufahamika mbinguni kabla ya hapo. Lusifa mwenyewe mara ya kwanza hakuifahamu asili halisi ya hisia zake. Ilipothibitika kuwa kutondhika kwake hakukuwa na msingi, Lusifa alishawishika kwamba madai ya Mungu yalikuwa ya haki na kwamba alipaswa kukiri mbele za mbingu yote. Endapo angelifanya hili, huenda angejiokoa yeye mwenyewe na malaika wengi. Ikiwa angehiari kumrudia Mungu, akiwa ameridhika kujaza nafasi ambayo angepewa, angerejeshwa katika ofisi yake. Lakini majivuno yalimzuia asijisalimishe. Alikuwa kuwa hakuwa na haja natoba, na akajitoa kikamilifu katika pambano kuu dhidi ya Mwumbaji wake. TK 307.2
Nguvu zote za akili zake zenye ubunifu sasa zilielekezwa kwenye udanganyifu, ili apate kuungwa mkono na malaika. Shetani alikuwa analalamika kuwa alihukumiwa isivyo halali na kwamba uhuru wake ulizuiwa. Baada ya kuyapotosha maneno ya Kristo alileta uongo wa moja kwa moja, akimshitaki Mwana wa Mungu kwamba alikuwa amemdhalilisha mbele ya wakazi wa mbinguni. TK 307.3
Wote ambao hakuweza kuwachochea wawe upande wake aliwashtaki kuwa hawakuyajali matakwa ya viumbe wa mbingum. Aliishia kuipotosha tabia ya Mwumbaji. Ilikuwa ni sera yake kuwafadhaisha malaika kwa hoja ngumu juu ya makusudi ya Mungu. Kila kitu rahisi alikifunika kwenye usiri, na kwa kutumia upotoshaji wenye ustadi akazitia mashaka kauli za Mungu zilizo wazi kabisa. Nafasi yake ya juu aliyokuwa nayo ikatoa msukumo kwa malalamiko yake. Wengi waliungana naye katika uasi. TK 307.4