Tumaini Kuu

187/254

Sura Ya 29 - Kwa Nini Dhambi Iliruhusiwa?

Wengi huiona kazi ya uovu pamoja na huzuni, na namna yake ya kutelekeza, na kuuliza ni kwa namna gani hili linaweza kuwepo chini ya enzi ya yule ambaye hana ukomo wa hekima, uwezo, na upendo. Wale wanaopendelea kuona mashaka huchukulia hicho kama kisingizio cha kuyakataa Maandiko Matakatifu. Mapokeo na tafsiri potovu vimetia giza fundisho la Biblia juu ya tabia ya Mungu, asili ya serikali yake, na kanuni anazotumia anaposhughulikiadhambi. TK 305.1

Haiwezekani kuelezea chanzo cha dhambi ili kutoa sababu ya kuwepo kwake. Lakini mengi yanaweza kufahamika juu ya chanzo na hatima ya tabia ya dhambi ili kubainisha kikamilifu haki na ukarimu wa Mungu. Mungu, kwa namna yoyote ile hahusiki na kuwepo kwa dhambi; hakukuwa na uondoaji kiholela wa neema ya Mungu, hakukuwa na upungufu katika serikali ya Mungu, uliotoa nafasi kwa uasi. Dhambi ni kitu kiiichojipenyeza ambacho uwepo wake hauna sababu inayoweza kutolewa. Kuitolea udhuru ni kuitetea. Endapo udhuru wake ungepatikana, ingekoma kuwa dhambi. Dhambi ni matokeo ya utendaji wa kanuni inayopingana na sheria ya upendo, ambayo ni msingi wa serikali ya Mungu. TK 305.2

Kabla ya kuingia kwa uovu kulikuwa na amani na furaha katika ulimwengu wote. Upendo kwa Mungu lilikuwa ndilo jambo kubwa kabisa, upendo kwa wengine haukuwa na upendeleo. Kristo Mwana pekee wa Mungu alikuwa mmoja na Baba, wa milele katika asili, katika tabia, na katika makusudi-nafsi pekee ambayo ingeingia katika mashauri yote na makusudi ya Mungu. “Katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni ...ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka.” Wakolosai 1:16. TK 305.3

Sheria ya upendo ikiwa ndiyo msingi wa serikali ya Mungu, furaha ya viumbe vyote ilikuwa inategemea hiari yao juu ya kanuni zake za haki. Mungu hafurahishwi na utii wa kulazimishwa, na huwapatia wote uhuru wa dhamiri, ili wamtolee huduma ya hiari. TK 305.4

Lakini alikuwepo mmoja aliyechagua kuupotosha uhuru huo. Dhambi ilianzia kwake, yeye ambaye alimfuatia Kristo, kwa kuheshimiwa sana na Mungu. Kabla ya anguko lake, Lusifa alishika nafasi ya kwanza kati ya makerubi wafunikao, mtakatifu, asiye na unajisi. “Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako... Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako...Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako.” “Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.” “Nawe ulisema... Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano...Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” Ezekieli 28:12-17; 28:6; Isaya 14:13-14. TK 306.1

Akiitamani heshima ambayo Baba alikuwa anaitoa kwa Mwaawe, mkuu huyu wa malaika, aliutamani uwezo ambao ulikuwa ni haki ya Kristo pekee kuwa nao. Hali ya kutoelewana iliharibu amani ya mbinguni. Kujiinua nafsi kuliamsha dalili za uovu ndani ya mioyo ambayo kwayo utukufu wa Mungu ulikuwa jambo la kwanza. Mabaraza ya mbinguni yalihojiana na Lusifa. Mwana wa Mungu alimweleza juu ya uzuri na haki ya Mwumbaji na asili takatifu ya sheria yake. Kwa kuiacha, Lusifa alikuwa anamvunjia heshima Mwumbaji wake na kujiletea uangamivu wake mwenyewe. Lakini onyo hilo liliamsha upinzani. Lusifa aliruhusu wivu aliokuwa nao dhidi ya Yesu kushinda. TK 306.2

Majivuno yalikuza shauku ya kutaka mamlaka ya juu. Heshima za juu alizotunukiwa Lusifa hazikumsukuma kumshukuru Mwumbaji. Alikuwa anatamani kuwa sawa na Mungu. Na bado Mwana wa Mungu alikuwa ndiye Mwenye enzi aliyetambuliwa mbinguni, mwenye uwezo na mamlaka pamoja na Baba. Katika mabaraza yote ya Mungu, Kristo alikuwa mshiriki, lakini Lusifa hakuruhusiwa kuingia kwenye makusudi ya Mungu. “Kwa nini?” Aliuliza huyu malaika mwenye nguvu, “Kristo awe na mamlaka ya juu? Ni kwa nini ameheshimiwa hivyo kupita Lusifa? TK 306.3