Tumaini Kuu

186/254

Hatima ya Wote Kuamuliwa

Wakati wa matazamio utamalizika muda mfupi kabla ya kutokea kwa Bwana katika mawingu ya mbinguni. Akiutazamia wakati huo, Yesu atatangaza: “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.”Ufunuo 22:11, 12. TK 303.3

Wanadamu watakuwa wakipanda na kujenga, wakila na kunywa, wote bila kujua kuwa uamuzi wa mwisho umekwisha kutolewa katika hekalu la mbinguni. Kabla ya gharika, baada ya Nuhu kuingia ndani ya safina, Mungu alimfungia ndani na waovu aliwafungia nje; lakini kwa siku saba watu walikuwa wanaendelea na maisha yao ya kupenda anasa na walikuwa wanadhihaki maonyo juu ya hukumu. Mwokozi anasema, “Ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” Saa ya kuweka hatima ya kila mwanadamu itakuja kimya kimya, bila kuonekana, kama mwivi wa usiku wa manane, “Kesheni basi... asije akawasili ghafula akawakuta mmelala” Mathayo 24:39; Marko 13:35, 36. TK 303.4

Wale ambao baada ya kuchoshwa na kukesha, wanageukia kwenye vivutio vya ulimwengu, hali yao ni ya hatari. Wakati mfanyabiashara akiwa ametopea katika kufukuzia faida, wakati mpenda anasa akiwa anatafuta kujifurashisha, wakati binti mwanamitindo akiyapangaa mapambo yake-huenda ikawa katika saa ile, hakimu wa dunia yote atatoa tamko lisemalo: Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.” Danieli 5:27. TK 304.1