Tumaini Kuu
Maombezi ya Kristo
Huduma ya Kristo ya upatanisho kwa niaba ya mwanadamu katika hekalu la mbinguni; ni ya muhimu katika mpango wa ukombozi kama kilivyokuwa muhimu kifo chake msalabani. Kwa kifo chake, aliianza ile kazi ambayo alipaa kwenda kuikamilisha mbinguni. Kwa imani inatupasakuingia ndani ya pazia, “alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu” Waebrania 6:20. Pale, nuru kutoka msalabani imeakisiwa. Pale ndipo tunapopata utambuzi ulio wazi kuhusu siri za ukombozi. TK 302.2
“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.” Mithali 28:13. Kama wale wanaotoa visingizio kwa ajili ya dhambi zao wangeona namna Shetani anavyomdhihaKikristo kwa sababu ya mwenendo wao; wangeungama dhambi zao na kuziondoakuzitupa mbali. Shetani anajitahidi kuidhibiti akili yote, na anajua kwamba kasoro zikiendekezwa, yeye atafanikiwa. Kwa hiyo anadumu kutafuta namna ya kuwadanganya wafuasi Wakristo kwa maneno ya hila na yenye kufisha ambayo ni vigumu kwao kuyashinda. Lakini Yesu alitangaza kwa wote ambao wangemfuata: “Neema yangu yakutosha” “Nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” 2Wakorintho 12:9; Mathayo 11:30. Hebu wasiwepo watu wanaouona upungufu wao kuwa hautibiki. Mungu atawapa imani na neema ili waushinde. TK 302.3
Sasa tunaishi katika siku ile kuu ya upatanisho. Wakati kuhani alipokuwa anafanya upatanisho kwa Waisraeli, iliwapasa wote wazitaabishe nafsi zao kwa kutubu dhambi zao. Kwa namna ile ile, wale wote ambao wanataka majina yao yabaki kwenye kitabu cha uzima wanatakiwa wazitaabishe nafsi zao mbele za Mungu kwa toba ya kweli. Kunatakiwa kuwepo na uchunguzi wa kina wa moyo. Ile roho isiyokuwa na kusudi maalum, ambayo imeendekezwa na wengi haina budi kuwekwa mbali. Kuna vita vya dhati kwa wote wanaotaka kuishinda mielekeo yao inayopambana ili kuwashinda. Kila mmoja ni lazima akutwe bila “ila wala kunyanzi, wala lo lote kama hayo.” Waefeso 5:27. TK 303.1
Katika wakati huu juu ya mengine yote, yapasa kila nafsi isikilize maagizo ya Mwokozi: “Kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.” Marko 13:33. TK 303.2