Tumaini Kuu

184/254

Ubinafsi Uliofichwa Wafunuliwa

Ubinafsi uliofichwa, unaonekana wazi ndani ya vitabu vya mbinguni. Ni mara nyingi kiasi gani wakati, wazo, na nguvu ambavyo ni mali ya Kristo alikuwa amepewa Shetani? Wafuasi wanaomkiri Kristo wametopea katika kutafuta mahitaji ya kidunia ama kufurahia anasa za dunia. Pesa , muda na nguvu hutumika kwaajili ya kujionesha na kujifurahisha nafsi; na muda mfupi hutengwa kwa ajili ya maombi, kuyachunguza Maandiko, na kuungama dhambi. TK 301.3

Shetani anabuni mipango isiyo na idadi ili aijaze kwenye akili zetu. Mdanganyifu mkuu anuchukia ukweli mkuu unaoifunua kafara ya upatanisho na Mpatanishi mwenye nguvu. Jambo kubwa kwake ni kuzichepua akili kutoka kwa Yesu. TK 301.4

Wale wanaotaka kushiriki matunda ya upatanisho wa Mwokozi yapasa wasiruhusu chochote kijiingize katika wajibu wao wa kukamilisha utakatifu katika kicho cha Mungu. Badala ya kutumiwa kwa kujifurahisha ama kutafuta mapato, muda wa thamani ungetakiwa utolewe kwa ajili ya kujifunza kwa maombi Neno la Kweli.. Somo la Patakatifu na Hukumu ya Upelelezi ni lazima yaeleweke kwa uwazi. Ni hitaji la wote kufahamu nafasi na huduma ya Kuhani wao Mkuu. Vinginevyo haitawezekana kuwa na imani ambayo ni muhimu kwa wakati huu. TK 301.5

Patakatifu pa mbinguni ni kiini cha kazi ya Kristo kwa niaba ya wanadamu. Inamhusu kila mwanadamu anayeishi duniani. Inaufunua mpango wa ukombozi, na kutuleta hadi kwenye kufungwa kwa shindano kati ya haki na dhambi. TK 302.1