Tumaini Kuu

183/254

WakatiUIioamuIiwa

Katika muda uliopangwa-kumalizika kwa siku 2300 mwaka 1844, kazi ya upelelezi na kuzifuta dhambi ilianza. Dhambi zisizofanyiwa toba na kuachwa, hazitafutwa kwenye vitabu vya kumbukumbu. Malaika wa Mungu waliishuhudia kila dhambi na kuiandikisha. Dhambi inaweza kukataliwa, kufichwa ili baba, mama, mke, watoto, na washirika wengine wasijue; lakini imewekwa wazi mbinguni. Mungu hawezi kudaganywa na jinsi tunavyoonekano.. Hawezi kukosea. Wanadamu wanaweza kudanganywa na wale wenye mioyo miovu, lakini Mungu huyasoma maisha ya ndani. TK 300.5

Hili ni wazo nyeti sana! Mshindi mwenye nguvu hapa duniani, hana uwezo wa kuirudisha kumbukumbu yake ya siku moja. Matendo yetu, maneno yetu, na hata mambo ya siri, ingawa tumeyasahau, yatatushuhudia kutupatia haki ama kutuhukumu. TK 301.1

Katika hukumu matumizi ya kila talanta yatachunguzwa kwa makini. Ni kwa namna gani tumeutumia muda, kalamu zetu, sauti zetu, pesa zetu, na mvuto wetu? Ni kitu gani tumemfanyia Kristo kupitia kwa maskini, wanaoteseka, yatima, ama wajane? Tumeufanyia nini ukweli na nuru tuliyopewa. Ni ule upendo tu uliooneshwa kwa matendo utakaohesabiwa. Upendo pekee yake, kwa mtazamo wa mbinguni, hulifanya kila tendo kuwa la thamani. TK 301.2