Tumaini Kuu

122/254

Sura Ya 19 - Kwa Nini Matumaini Yalivunjika?

Tangu kizazi hata kizazi,kazi ya Mungu, huonesha mfanano wa ajabu m katika kila matengenezo makubwa au harakati za kidini. Kanuni za Mungu za kushughulika na wanadamu ni zile zile siku zote. Harakati muhimu za sasa zinafanana na zile zilizopita na mambo yaliyolipata kanisa katika zama zilizopita yana mafundisho kwa ajili ya wakati wetu. TK 219.1

Kwa njia ya Roho wake Mtakatifu Mungu kwa huwaongoza watumishi wake wa duniani kwa namna ya pekee, kuendeleza kazi ya wokovu. Wanadamu ni vyombo katika mkono wa Mungu. Kila mmoja amepewa kiasi cha nuru inayotosha kufanya kazi aliyopewa. Lakini hakuna mwanadamu aliyewahi kuyaelewa kikamilifu makusudi ya Mungu katika kazi iliyopo kwa wakati wake. Wanadamu huwa hawauelewi kwa upana wote ujumbe wanaoutangaza kwa jina lake. Hata manabii hawakuwa wanaelewa kikamilifu ufunuo waliokuwa wamepewa. Maana yake ilitarajiwa kufunuliwa kutoka kizazi hadi kizazi. TK 219.2

Petro asema: Katika habari za wokovu huo “manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho Wakristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walihudumu katika mambo hayo.” (I Pet. 1:10-12). Ni somo muhimu jinsi gani kwa watu wa Mungu katika Zama za Ukristo! Watakatifu hao wa Mungu, “walitafuta na kuchunguza kwa makini” kuhusu ufunuo uliokuwa umetolewa kwa ajili ya vizazi vilivyokuwa havijazaliwa bado. Hili ni kemeo kubwa kiasi gani kwa hali ya kutokujali na kupenda dunia, kuridhika na kutamka kuwa unabii hauwezi kueleweka. TK 219.3

Siyo mara chache akili za watumishi imara wa Mungu hupofushwa na mapokeo na mafundisho ya uongo kiasi kwamba wanaweza kuelewa kwa sehemu tu mambo yanayofunuliwa katika Neno lake. Hata Mwokozi alipokuwa nao, wanafunzi Wakristo walikuwa na dhana iliyopendelewa na wengi ya kuwa Masihi ni mfalme wa kidunia ambaye angeikweza Israeli na kuwa dola ya ulimwengu. Hawakuwa wanaelewa maneno yake yaliyokuwa yanatabiri juu ya mateso na kifo chake. TK 219.4