Tumaini Kuu

121/254

Wabishi na Wasioamini

Kristo alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa watu wa siku za Nuhu, hawakutambua, “hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu” (Mathayo 24:39). Wakati wanadai kuwa watu wa Mungu wanajiunga na ulimwengu; wakati anasa za ulimwengu zinakuwa anasa za kanisa, wakati wote wakitarajia miaka mingi ya ustawi kiulimwengu—ndipo matumaini yao ya bandia yatakapokoma ghafla kama radi inavyopiga. Kama vile Mungu alivyomtuma mtumishi wake kuuonya ulimwengu kuhusu Gharika iliyokuwa inakuja, ndivyo alivyotuma wajumbe wake wateule kuutangaza ukaribu wa hukumu ya mwisho. Kama vile watu wa kizazi cha Nuhu walivyocheka wakibeza utabiri wa mhubiri huyo wa haki, ndivyo wengi wa wale waliokuwa wanaodai kuwa watu wa Mungu wakati wa Miller walivyokejeli maneno hayo ya onyo. TK 217.1

Hakuwezi kuwa na ushahidi wa uhakika zaidi kuwa makanisa yalikuwa yamemwacha Mungu kuliko chuki iliyochochewa na ujumbe huu uliotoka mbinguni. TK 217.2

Wale waliolikubali fundisho la ujio wa Yesu waliona kuwa wakati wa kufanya uamuzi ulikuwa umefika. Mbingu iliwakaribia na wakajiona kuwa na hatia mbele za Mungu.” 208 Wakristo walifanywa waone kuwa muda ulikuwa mfupi, na mambo waliyokuwa wanapaswa kuyafanya kwa ajili ya wanadamu wenzao yalipaswa kufanyika haraka. Umilele ulionekana ukifunguka mbele zao. Roho wa Mungu alitia nguvu kusihi kwao wakiwaandaa watu kwa ajili ya siku ya Mungu. Maisha yao ya kila siku yalikuwa kemeo kwa washiriki wa kanisa waliokuwa hawajajiweka wakfu. Hawa hawakutaka kubughudhiwa katika starehe zao, kutafuta pesa, na kutafuta heshima ya kidunia. Hatimaye kukawa na upinzani dhidi ya imani juu ya ujio. TK 217.3

Wapinzani walijaribu kukatisha tamaa ya uchunguzi wa unabii kwa kufundisha kuwa unabii ulikuwa utiwa muhuri. Kwa hiyo, Waprotenstanti walifuata nyayo za Wakatoliki. Makanisa ya Kiprotestanti yalidai kwamba, sehemu muhimu ya Neno, sehemu inayohusu hasa wakati wetu, ilikuwa haieleweki. Wachungaji walidai kuwa vitabu Danieli na Ufunuo vilikuwa mafumbo yasizoeleweka. TK 217.4

Lakini Kristo aliwaelekeza wanafunzi wake kwenye maneno ya nabii Danieli, “Asomaye na afahamu” (Mathayo 24:15). Kitabu cha Ufunuo kinapaswa kueleweka. “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwapo upesi .... Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufunuo 1:1-3. TK 218.1

“Heri asomaye”—wapo ambao hawatasoma; “na wale wasikiao”—wapo wasiotaka kusikia cho chote kuhusu unabii; “na kuyashika yaliyoandikwa humo”—wapo wengi wanaokataa kuyashika maagizo yaliyotolewa katika kitabu cha Ufunuo; kati yao hakuna aliye na haki ya kudai baraka zilizoahidiwa. TK 218.2

Mwanadamu anawezaje kuthubutu kufundisha kuwa kitabu cha Ufunuo hakiwezi kueleweka na wanadamu? Ni siri iliyofunuliwa, yaani kitabu kilichofunguliwa. Kitabu cha Ufunuo kinaelekeza akili kwenye kitabu cha Danieli. Vyote viwili vintotoa maelezo muhimu juu ya matukio yanayoambatana na kufungwa kwa historia ya ulimwengu. TK 218.3

Yohana aliziona hatari, migongano, na ukombozi wa mwisho wa watu wa Mungu. Aliuandika ujumbe wa mwisho utakaokomaza mavuno ya nchi, ama kwa ajili ya ghala la mbinguni ama kwa ajili ya moto wa maangamizi, ili wale wanaouacha ukosefu waelezwe juu ya hatari na migongano iliyo mbele yao. TK 218.4

Ni kwa nini basi kuna ujinga ulitapakaa pote kuhusu sehemu hii muhimu ya Maandiko Matakatifu? Ni matokeo ya juhudi za makusudi za mkuu wa giza kuficha jambo ambalo litafichua uongo wake. Kwa sababu hiyo, Kristo ambaye ndiye afunuaye, akiiona kabla vita dhidi ya Ufunuo, aliahidi baraka kwa wote watakaosoma, watakaosikia, na kuushika unabii huu. TK 218.5