Tumaini Kuu
Shauku na Kutokuamini
Shauku ilizidi kuongezeka. Kutoka makumi na mamia, makanisa yaliongezeka hadi kuwa na maelfu ya washiriki. Lakini baada ya muda, upinzani ulijitokeza dhidi ya waongofu hawa, na makanisa yakaanza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale waliokuwa wakipokea maoni ya Miller. Jambo hili lilihitaji kujibiwa na Miller kwa maandishi: “Kama tumekosea, tafadhali mtuoneshe tulipokosea. Tuonesheni kosa letu kutoka kwenye Neno la Mungu; tumebezwa kiasi cha kutosha; kejeli haziwezi kutushawishi kuwa tumekosea; Neno la Mungu tu ndilo liwezalo kubadili maoni yetu. Uamuzi wetu umefanyika kwa umakini na maombi, kama tulivyouona ushahidi katika Maandiko.” 207 TK 216.2
Wakati uovu wa watu waliokuwa wanaishi kabla ya Gharika ulipomfanya Mungu alete gharika duniani, kwanza aliwajulisha azma yake. Kwa miaka 120 lilitangazwa onyo kwa ajilinya kutubu. Walimbeza mjumbe wa Mungu. Ikiwa ujumbe wa Nuhu ulikuwa sahihi, ni kwa nini ulimwengu wote usiuone na kuuamini? Madai ya mtu mmoja dhidi ya hekima ya maelfu! Hawakutaka kuliamini lile onyo wala kutafuta hifadhi katika safina. TK 216.3
Wafanya dhihaka walionesha mfuatano wa majira usiobadilika, anga la samawi ambalo lilikuwa halijawahi kudondosha mvua. Kwa dharau, mhubiri wa haki walimwita mwendawazimu mwenye shauku. Waliendelea na njia zao mbaya kwa jeuri zaidi kuliko mwanzo. Lakini hukumu za Mungu zilimwagwa juu ya walioikataa rehema katika wakati uliokuwa umepangwa. TK 216.4