Tumaini Kuu
Utabiri Watimia
Katika muda uliokuwa umetajwa, Uturuki ilikubali kuwa chini ya ulinzi wa majeshi ya umoja ya Ulaya, hivyo kujiweka yenyewe chini ya mataifa ya Kikristo. Tukio hilo lilitimiza unabii huo kwa usahihi. Watu wengi waliziamini njia za kufasili zilizokuwa zinatumiwa na Miller na wenzi wake. Wasomi na wakuu waliungana na Miller katika kuhubiri na kuchapisha maoni yake. Tangu mwaka 1840 hadi 1844 kazi ilipanuka kwa kasi. TK 215.1
William Miller alikuwa na uwezo mkubwa kiakili, na aliongezea hekima za mbinguni kwa kuwa na uhusiano na Chanzo cha Hekima. Aliheshimiwa po pote ambapo unyofu na ubora wa maadili ulikuwa unathaminiwa. Akiwa na unyenyekevu wa Kikristo, alikuwa msikivu na rafiki wa wote, akiwa tayari kuwasikiliza wengine na kupima hoja zao. Alizipima nadharia zote kwa Neno la Mungu, na busara zake na ujuzi wake wa Maandiko vilimwezesha kupinga uongo. TK 215.2
Lakini, kama ilivyokuwa kwa wanamatengenezo wa mwanzo, ukweli aliokuwa anaufundisha haukupokelewa na walimu mashuhuri wa kidini. Kwa vile walimu hao wa kidini hawakuweza kudumisha nafasi yao kwa Maandiko, waligeukia mafundisho ya wanadamu, desturi za Mababa. Lakini Neno la Mungu lilikuwa ushuhuda pekee uliokuwa unakubalika na wahubiri wa ukweli wa kuja kwa Yesu. Kejeli na dhihaka zilitumiwa na wapinzani ili kuwaharibia sifa wale waliokuwa wanafurahia kurudi kwa Bwana wao na walikuwa wakijitahidi kuishi maisha matakatifu na kuwaandaa wengine kwa ajili ya ujio wake. Ilifanywa ionekane kuwa ni dhambi kuchunguza unabii wa kurudi kwa Kristo na wa mwisho wa dunia. Hivyo huduma iliyopendwa na wengi ilihafifisha imani katika Neno la Mungu. Mafundisho yao yaliwafanya watu kuwa waovu, na wengi walihalalisha kuenenda kwa kuzifuata tamaa za watu waovu. Halafu waasisi wa uovu huo, walipeleka lawama zote kwa Waadventista. TK 215.3
Huku akijaza wasikilizaji makini katika majumba, jina la Miller lilitajwa mara chache katika vyombo vya habari vya kidini isipokuwa kwa kubezwa au shutuma. Waovu, wakiwa wamehamasishwa na walimu wa kidini, waligeukia kejeli za kukufuru(p. 210) dhidi yake pamoja na kazi yake. Mzee huyu mwenye mvi aliyekuwa ameacha makazi yake mazuri na kusafiri kwa gharama zake mwenyewe kwa ajili ya kuupelekea ulimwengu onyo la hukumu iliyokuwa inakaribia, alishutumiwa kwamba alikuwa na itikati kali. TK 216.1