Tumaini Kuu
“Nyota Zitaanguka”
Mwaka 1833 ishara ya mwisho kati ya zile zizokuwa zimeahidiwa na Mwokozi kama dalili za kuja kwake itokea: “Nyota zitaanguka kutoka mbinguni.” Naye Yohana katika Ufunuo anasema: “Na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi” (Mathayo 24:29; Ufunuo 6:13). Unabii huu ulitimia kwa namna ya ajabu kwa anguko kuu la vimondo Novemba 13, 1833, onesho la ajabu la kuanguka kwa nyota lililochukua muda mrefu kabisa kuliko yote yaliyowahi kuandikwa katika kumbukumbu. “Hakujawahi kunyesha mvua kubwa kama ile ya vimondo vilivyoanguka chini; mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini, hali ilikuwa ile ile. Kwa kifupi, anga lote lilikuwa katika hekaheka. ... Tangu saa nane usiku mpaka kulipopambazuka kabisa, anga lilikuwa safi bila mawingu, onesho la vitu vinavyong’ara lilidumu katika anga lote.” 203 TK 213.4
“Ilionekana kana kwamba nyota zote mbinguni zimekutana katika upeo wa anga, na zilikuwa zinafyatuka kwa pamoja kwa kasi ya radi, zikielekea kila upande lakini zilikuwa haziishi—maelfu yalifuata upesi katika njia ya maelfu kana kwamba zilikuwa zimeumbwa kwa ajili ya tukio hilo.” 204 TK 214.1
“Taswira sahihi zaidi ya mtini unaopukutisha mapooza yake unapotikiswa na upepo mkali, ambayo ilikuwa haiwezekani kuitazama.” 205 TK 214.2
Katika jarida la Biashara la New York la Novemba 14, 1833 kulitokea makala ndefu kuhusu hali hiyo: “Hakuna mwanafalsafa au mwanazuoni aliyewahi kusimulia au kuandika juu ya tukio kama lile la jana asubuhi. Nabii mmoja alilitabiri kwa usahihi karne kumi na nane zilizopita. kama tutakuwa na tatizo kuelewa kwamba kuanguka kwa nyota inamaanisha nyota zinazoanguka; maana pekee ambapo inawezekana kwa jambo hili kuwa kweli kama lilivyokuwa limeandikwa.” TK 214.3
Kwa njia hiyo ilidhihirishwa dalili ya mwisho katika dalili za kuja kwake ambazo Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.” (Mathayo24:33). Wengi walioshuhudia kuanguka kwa zile nyota, waliona jambo hilo kama tangazo la hukumu illiyokuwa inakuja. TK 214.4
Mwaka 1840 utimilifu mwingine wa unabii ulivuta usikivu mkuu wa watu. Miaka miwili kabla ya hapo, Josiah Litch aliandika ufafanuzi wa Ufunuo 9, ikitabiri kuanguka Himaya ya Ottoman mwaka 1840, mnamo mwezi wa nane.” Siku chache tu kabla ya kutimia kwa unabii huo aliandika: “Itakoma Agosti 11, 1840, ambapo himaya ya Ottoman huko Constantinople inatarajiwa kuvunjika.”206 TK 214.5