Tumaini Kuu
“Nenda Kauambie Ulimwengu”
“Wakati nikiwa kwenye shughuli zangu,” alisema, “iliendelea kusikika katika masikio yangu, ‘Nenda uuambie ulimwengu juu ya hatari inayoukabili.’ Aya hii iliindelea kunijia: ‘Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe utajiokoa roho yako.’ Ezekieli 33:8, 9. Nilijihisi kuwa endapo waovu wataonywa kikamilifu; wengi wao watatubu; na kama hawataonywa, damu yao itatakiwa mkononi mwangu.” 202 Maneno hayo yalikuwa yanajirudia rudia katika akili yake. “Nenda kauambie ulimwengu; damu yao nitaitaka mikononi mwako.” Alisubiri kwa miaka tisa, jukumu hilo likimsumbua rohoni, hadi mwaka 1831 alipotangaza hadharani sababu za imani yake. TK 212.1
Wakati huo alikuwa na miaka hamsini, akiwa hana uzoefu wa kuhubiri hadharani, ila jitihada zake zilibarikiwa. Hotuba yake ya kwanza ilifuatiwa na uamsho mkuu wa kiroho. Familia nzima kumi na tatu, kasoro watu wawili tu, ziliongolewa. Aliombwa kwenda kuhubiri mahali pengine, na karibu kila mahali wadhambi waliongolewa. Wakristo waliamshwa na kujiweka wakfu kwa Mungu. Wenye mizaha na wasioamini Mungu wakaupokea ukweli wa Biblia. Hotuba zake za Neno la Mungu ziliamsha ari ya kiroho katika jamii na kupunguza kasi ya ukengeufu na anasa katika kizazi hicho. TK 212.2
Katika sehemu nyingi makanisa ya Kiprotestanti ya madhehebu karibu zote yalifungua milango yao kumruhusu ahutubie, na mialiko hiyo mara nyingi ilitoka kwa wachungaji wa makanisa hayo. Ilikuwa ni kanuni yake kutohutubia mahali ambapo hakupewa mwaliko, hata hivyo alijikuta hawezi kuhudumia hata nusu ya mialiko aliyokuwa anapewa. Wengi walishawishika juu ya uhakika na ukaribu wa kuja kwa Kristo na hitaji lao la kujiandaa. TK 213.1
Katika baadhi ya miji mikubwa, wauza pombe walibadili maduka kuwa vyumba vya mikutano; sehemu za kamari zilifungwa; makafiri na mafisadi walibadilika. Mikutano ya maombi ilianzishwa na madhehebu mbalimbali iliyofanyika karibu kila saa, wafanya biashara wakikusanyika wakati wa adhuhuri kwa ajili ya sala na sifa. Hakukuwa na burudani za kifujaji. Kazi yake, kama ilivyokuwa kazi ya wana-matengenezo wa awali, ilikuwa na mwelekeo wa kushawishi ufahamu na kuamsha dhamiri kuliko kusisimua hisia tu. TK 213.2
Mwaka 1833 William Miller alipewa hati ya kuhubiri kutoka Kanisa la Kibaptisti. Idadi kubwa ya wachungaji wa madhehebu yake waliridhika na kazi yake; aliendelea na kazi yake kwa idhini yao. Alisafiri na kuhubiri bila kukoma; japo alikuwa hana kipato cha kutosha kukidhi gharama za safari kufika maeneo yote aliyoalikwa. Hivyo juhudi zake za hadhara ziliathiri sana mali zake. TK 213.3