Tumaini Kuu

116/254

Hitimisho la Kushtusha

Pale mwanzoni Miller hakuwa na tumaini la kufikia hitimisho alilofikia sasa. Yeye mwenyewe hakuamini kwa urahisi matokeo ya uchunguzi wake.. Lakini ushahidi wa Maandiko ulikuwa wazi kiasi cha kushindwa kuuweka kando. TK 211.4

Mnamo 1818 alisadiki kwa dhati kuwa baada ya miaka ishirini na tano Yesu angerudi kuokoa watu wake, “sihitaji kueleza,” alisema Miller, “juu ya furaha iliyoujaza moyo wangu kwa taraja yenye furaha, wala shauku niliyo nayo kutaka kushiriki furaha ya waliokombolewa ...Oo ni kwa mng’ao na utukufu kiasi gani ukweli ulionekana!...“Swali lilimjia kwa nguvu kubwa kuhusiana na jukumu langu kwa ulimwengu, kwa mtazamo wa ushahidi uliougusa moyo wangu” 201 Alihitajika tu kuhisi kuwa ulikuwa ni wajibu wake kuwapatia wengine nuru aliyoipokea. Aliutazamia upinzani kutoka kwa kwa wale wasiomcha Mungu, lakini alikuwa na ujasiri kuwa Wakristo wangelifurahia tumaini la kukutana na Mwokozi . Alisita kulitoa taraja la ukombozi wenye utukufu, ulio karibu sana kutimizwa, asije akakosea na kuwapotosha wengine. Hivyo aliongozwa kupitia upya na kuufikiria kwa uangalifu kila ugumu ulioonekana katika akili yake. Miaka mitano aliitumia kupata usahihi wa msimamo wake. TK 211.5