Tumaini Kuu
Injili Iliyotolevva Kvva Ulimwengu
“Naye atafanya na kulithibisha agano kwa wengi kwa muda wa juma moja” Miaka saba ya mwisho ilitolewa kwa ajili ya Wayahudi. Wakati huu, kuanzia A.D. 27 mpaka A.D. 34, Kristo na wanafunzi wake walitangaza Injili ya mwaliko hasa kwa Wayahudi. Maelekezo ya Kristo yalikuwa “Msiende kwa mataifa na wala miji ya wasamaria msiingie, lakini nendeni kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, Mt 10: 56. TK 211.1
“Katikati ya juma ataikomesha sadaka na dhabihu” Katika A.D. 31, miaka mitatu na nusu baada ya ubatizo wake, Bwana wetu alisulubiwa. Katika kafara kuu iliyotolewa Kalvari, kielelezo kilikutana na kile kilicho halisi. Saadaka zote za kuteketeza na dhabihu za kila siku zilikoma. TK 211.2
Miaka 490 waliyopewa Wayahudi iliishia A.D 34, Wakati huo , kwa kitendo cha Baraza ya Kiyahudi la Sanhedrini taifa lilitia muhuri wa kuikataa Injili kwa kumwua Stefano na kuwatesa Wafuasi Wakristo. Kisha ujumbe wa wokovu ukatolewa kwa ulimwengu. Wanafunzi wakisukumwa na mateso walikimbia kutoka Yerusalemu ” Wakihubiri Injili kila mahali” Matendo ya Mitume 8:4. TK 211.3