Tumaini Kuu
Vipindi Viwili vya Wakati Vyaanza Pamoja
Lakini ni kutoka katika kitu gani vipindi hivi vilikatwa? Kwa sababu siku 2300 ndio kipindi pekee kilichotajwa katika sura ya 8, majuma sabini yatakuwa ni sehemu ya siku 2300. Vipindi viwili lazima vianze pamoja , majuma sabini kuanzia tarehe ya ” amri iliyotolewa” kuujenga upya Yerusalemu. Endapo tarehe ya amri hii ingeonekana, mahali pa kuanzia kwa siku 2300 pangekuwa ni hakika. TK 210.2
Tamko linapatikana katika sura ya saba ya kitabu cha Ezra,, likitolewa na mfalme Artashasta wa Uajemi mwaka 457 B.C. Wafalme watatu katika kuanzisha na kukamilisha amri, walizifanya ukamilifu uliohitajika na unabii kuwa ndio mwanzo wa siku 2300. Ukichukua miaka 457 BC wakati tamko lilipotolewa , kama tarehe ya “amri” kila maelekezo ya majuma sabini yalionekana kukamilika. (Angalia Kiambatisho) TK 210.3
“Tangu amri ya kuujenga upya na kuutengeneza Yerusalemu mpaka masihi aliye mkuu kutakuwa na majuma saba, na majuma sitini na tisa au miaka 483. Amri ya Artashasta ilikuwa ni katika majira ya kupukutisha majani 457 B.C Kuanzia tarehe hii miaka 483 inakwenda mpaka wakati wa kupukutisha majani AD 27 wakati ambao unabii ulitimizwa katika wakati wa kupukutisha majani A.D 7 Yesu Kristo alibatizwa na Yohana na kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu Baaada ya ubatizo wake alikwenda Galilaya “akihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu , akisema ,wakati umetimia.” Marko .1: 41: 15. TK 210.4