Tumaini Kuu

113/254

Kugundua Ratiba ya Unabii

Miller aliendelea kuuchunguza unabii, alikesha wakati wa usiku na mchana akijifunza unabii ulioonekana kuwa na umuhimu wa ajabu. Katika sura ya 8 ya Danieli hakupata dokezo la mahali zilipoanza kuhesabiwa siku 2300; malaika Gabriel, ambaye ijapokuwa aliamriwa kumsaidia Danieli kuelewa maono alimpa maelezo ya juu juu tu. Kwa kadiri mateso ya kuogofya ambayo yangelipata kanisa yalivyofunuliwa kwa nabii, hakuweza kuvumilia zaidi. Danieli “alizimia na akawa mgonjwa kwa siku kadhaa.” Naliyastaajabia yale maono lakini hakuna aliyefahamu.” Alisema. Danieli 8:27. TK 209.2

Bado Mungu alimwagiza mjumbe wake kuwa, “mfahamishe mtu huyu maono haya.” Kwa utii, malaika alirudi tena kwa Danieli, akisema; “nimetokea sasa ili nikupe akili upate kufahamu basi itafakari habari hii na kuyafahamu maono haya.” Jambo moja la muhimu katika sura ya 8 liliachwa bila maelezo ambalo ni siku 2300; kwa hiyo malaika, alianza tena maelezo akikazia hasa juu ya wakati: “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma sabini na katika majuma sitini na mawili kutajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya majuma sitini na mawili, masihi atakataliwa mbali atakuwa hana kitu; Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu.” Daniel 8:16-9:22, 23, 24-27. TK 209.3

Malaika alitumwa kwa Danieli kuelezea sehemu ambayo alikuwa hajaielewa -“Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Maneno ya kwanza ya malaika ni, “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu” Neno “kuamriwa” kiuhalisia linamaanisha “kuamriwa.” Majuma sabini, miaka 490 ingekatwa kwa ajili ya wayahudi. TK 210.1