Kutayarisha Njia

84/210

Sala na Kusoma Biblia ni Muhimu Ili Kufanya Uamuzi Ulio Bora

Kwamba imeanzishwa na Mungu, ndoa ni jambo takatifu; kamwe isingeingiwa kwa moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe, bila kujali wengine. Wale wanaotazamia hatua hii yawapasa kufikiri ukubwa wake kwa kicho na kuomba kwa bidii na kutafuta shauri kwa Mungu ili wapate kujua kama wamefuata njia yenye kupatana na mapenzi yake Mungu. Mafundisho yaliyotolewa katika neno la Mungu juu ya jambo hili yangefikiriwa kwa uangalifu. Mbinguni huangalia kwa furaha ndoa inayofanywa kwa haja ya kweli kupatana na maagizo ambayo yametolewa katika Biblia. KN 133.6

Kama kuna jambo ambalo lapasa kufikiriwa kwa makini na akili kamili zisizoharibika kwa tamaa, hilo ni jambo la ndoa. Ikiwa Biblia yatakikana kama mshauri, ni kabla ya kufanya hatua inayowafungamanisha watu pamoja maishani. Lakim, watu wengi wanavyoona ni kwamba katika jambo hili maoni ya moyoni hayana budi kuwa kiongozi, na kwa wengi mno wepesi wa kuvutwa na tamaa hushika usukani na kuwapeleka penye unaribifu fulani. Hapa ndipo mahali vijana wanapoonyesha upungufu wa akili kuliko katika jambo lo lote lingine; hapa ndipo wanapokataa kuhojiwa. Jambo la ndoa huelekea kuwa na nguvu za kupoteza akili juu yao. Hawajiweki chini ya Mungu. Akili zao zimerungwa minyororo, nao husonga mbele kwa siri, kana kwamba mipango yao yaweza kuingiliwa na mtu mwingine. KN 134.1

Wengi wanasafiri kwenda kwenye bandari ya hatari. Wanahitaji nahodha; lakini wanadharau kupokea msaada unaotakikana sana, wakiona moyoni kuwa ni wenye akili ya kutosha kuongoza jahazi lao wenyewe, wasifahamu kuwa limekaribia kugonga mwamba usioonekana ambao waweza kuwafanya wavun- KN 134.2

jikiwe na chombo chao cha imani na furaha Wasipokuwa wanafunzi hodari wa lile Neno (Biblia), watafanya makosa makubwa ambayo yataharibu furaha yao na ile ya wengine, kwa maisha haya na kwa yale ya wakati ujao pia. KN 134.3

Kama wanaume na wanawake wana mazoea ya kumwomba Mungu mara mbili kila siku kabla ya kulifikiri jambo la ndoa, yawapasa Kumwomba Mungu mara nne kila siku wakati wanapoitazamia hatua hii. Ndoa ni jambo ambalo litakuwa na mvuto na matokeo kwenye maisha yenu, ulimwenguni humu na katika ulimwengu ujao Ndoa zilizo nyingi za siku zetu na namna zinavyofanywa inazifanya ziwe mojawapo ya dalili za siku za mwisho. Wanaume kwa wanawake ni wakaidi, wasiosikia shauri la mtu, hata Mungu hawamjali katika neno hili. Dini imewekwa kando kana kwamba haihusiani hata kidogo na neno hili la dini tena lenye maana. KN 134.4