Kutayarisha Njia
Upendo ni Kipaji cha Thamani Kitokacho kwa Yesu
Upendo ni kipaji cha thamani, tupatacho kutoka kwa Yesu. Upendo safi na mtakatifu siyo kuona moyoni, bali ni kanuni. Wale ambao wamevutwa na upendo wa kweli si wapumbavu wala vipofu. KN 132.4
Upendo halisi, wa kweli, wa moyoni, ni safi na adimu sana. Kitu hiki cha thamani chapatikana kwa shida. Wengine huita tamaa mbaya upendo. KN 132.5
Upendo wa kweli ni kanuni bora takatifu, tofauti kabisa na namna ya upendo unaoamshwa na tamaa, ambao hufa mara ukijaribiwa vikali. KN 132.6
Upendo ni mmea unaokua vizuri mno, nao hauna budi kukuzwa na kulishwa. Moyo wa upendo, maneno ya kweli na upendo, yatafanya watu wa nyumba kuwa wenye furaha na kutoa mvuto wenye kuinua hadhi kwa wote walio mahali wanapoweza kufikiwa na mvuto wao. KN 133.1
Huku upendo safi ukimwingiza Mungu katika mipango yake vote, na kupatana kabisa na Roho wa Mungu, tamaa mbaya itakuwa kaidi isiyosikia shauri la mtu, ya kipumbavu, yenye kudharau amri zote, nayo itafanya kitu ilichokichagua kuwa mungu wa sanamu. Katika tabia vote ya mtu mwenye upendo wa kweli, neema ya Mungu itadhihirishwa. Adabu, utovu wa anasa, unyofu, adili, na dini itafanywa kila hatua inayofanywa kuielekea ndoa. Wale ambao wametawaliwa hivi hawatamezwa na mazungumzo waliyo nayo, na kupoteza moyo wa kupenda mkutano na sala na ibada ya dini. Moyo wao wa bidii kwa Neno la Mungu hautakuwa kwa sababu ya kutojali nafasi na majaliwa waliyopewa na Mungu. KN 133.2
Upendo ambao hauna msingi bora ila kundhisha tu tamaa za mwili utaKuwa mgumu usiosikia shauri la mtu, kipofu, na usiozuilika. Heshima, kweli, na kila uwezo bora wenye kuinua hali ya moyo huwekwa chini ya utumwa wa tamaa mbaya. Mtu ambaye amefungwa katika minyororo ya namna hii huku akipotewa na akili mara nyingi ni kiziwi asiyesikisa sauti ya akili na dhamiri ya moyoni; majadiliano wala maombi hayawezi kumwongoza kuona ujinga wake. KN 133.3
Upendo wa kweli siyo tamaa mbaya yenye nguvu, kali, ya harahara. Kinyume chake, ni mtulivu na utokao moyoni kwa ndani. Unatazama siyo mambo ya juu juu tu, nao huvutwa tu na tabia. Ni wa akili na busara, na ni upendo wa kweli, wenye kudumu. KN 133.4
Ukiinuliwa au kukuzwa vema na kuachana na mambo ya ashiki na tamaa za mwili, upendo huwa mtakatifu, nao hudhihirishwa katika maneno na matendo. Mkristo hana budi kuwa na wema na upendo mtakatifu tu usio na pupa au masumbufu; ufidhuli, na tabia za kijinga zimepasa kulainishwa na neema ya Kristo. KN 133.5