Kutayarisha Njia

82/210

Mambo ya Kuangalia kwa Mume Anayetazamiwa

Kabla hajatoa mkono wake kutia ndoa, kila mwanamke apaswa kuuliza kama mwanamume anayekaribia kuungana naye maisha yake yote anafaa. Habari zake za siku zilizopita zikoje? Maisha yake ni safi? Mapenzi anayoonyesha ni bora, ya tabia njema, au ni mahaba ya ovyo tu? Anayo tabia itakayomfanya kuwa mwenye furaha? (Mkewe) aweza kupata amani na raha halisi akiwa nae? Ataruhusiwa kuendelea na tabia zake, au itambidi kuyatupilia mbali yake na dhamiri ya moyo wake kwa sababu ya mamlaka ya mumewe? Je, aweza kuyaheshimu madai ya Mwokozi kama wajibu ulio mkubwa kuliko mambo yo vote mengine? Mwili na roho, mawazo na makusudi, yataweza kuhifadhiwa katika hali safi na takatifu? Maswali haya yana maana sana iuu ya hali bora ya kila mwanamke anayetarajia maisha ya unyumba. KN 131.5

Kila mwanamke anayetamani kuwa na unyumba wenye raha na amani apendaye kuepukana na taabu na huzuni za baadaye, hujiuliza maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa mapenzi. Je, mpenzi wangu anaye mama? Tabia ya mama yake ikoje? Anaufahamu wajibu wake kwa mamaye? Anajali haja na furaha ya mamaye? Ikiwa hamjali wala kumheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe? Shani ya arusi itakapokuwa imekwisha, atadumu kunipenda? Atanivumilia kwa makosa yangu, ama atakuwa akinitoa makosa mara kwa mara, mgomvi na mkali? Mapenzi ya kweli yatasamehe makosa mengi; upendo hautayaona. KN 132.1

Msichana amkubali kama mwenzake wa maisha mtu yule tu aliye na tabia safi ya utu, mwenye bidii, mwangalifu mwenye heshima, mwaminifu na mnyofu, mwenye kumpenda na kumcha Mungu. KN 132.2

Epukana na wafidhuli au wale wasio na adabu. Epukana na mvivu; epukana na mtu mwenye kuyadhihaki mambo matakatifu. Usishirikiane na mtu mwenye kutumia maneno mabaya yasiyo ya dini, au mzoefu wa kunywa japo bilauri moja ya pombe. Usisikilize posa za mtu asiyefahamu wajibu wake kwa Mungu. Neno la kweli, safi, ambalo hutakasa roho ya mtu litakupa moyo mkuu kujitenga na kuachana na rafiki mwenye kupendeza sana ambaye wajua hampendi wala kumcha Mungu, ama haiui lo lote juu ya kanuni za haki halisi. Twaweza siku zote kuvumilia udhaifu wa rafiki na ujinga wake lakini kamwe hatuwezi kustahimili maovu yake. KN 132.3