Kutayarisha Njia

194/210

Wakati wa Kawaida wa Kula Chakula

Baada ya kula mlo wa kawaida, yafaa tumbo lipewe nafasi va kupumzika muda wa saa tano. Kipande cho chote cha chakula kisitiwe tumboni mpaka mlo mwingine. Katika nafasi hiyo tumbo litafanya kazi yake, kisha litakuwa tayari kupokea chakula kingine zaidi. 17 KN 253.3

Kula kwa wakati usiobadilika ni jambo lipasalo kuangaliwa sana. Haifai kula cho chote kati ya milo, pipi, njugu, matunda, wala chakula cha namna yo yote. Kutokuwa na saa za kawaida za kula chakula huharibu hali njema ya afya ya viungo vinavyoyeyusha chakula tumboni, hata kuidhuru afya na raha. Pia watoto wakifika mezani, hawapendezwi na vyakula bora; tamaa zao hukitamani kile ambacho ni chenye kuwadhuru. 18 KN 253.4

Tulalapo, yafaa tumbo liwe limefanya kazi yake yote, ili lipate kupumzika pamoja na viungo vinginevyo vya mwili. Hasa kwa watu wanaofanya kazi za kuketi, ni vibaya kula chakula usiku sana. KN 253.5

Mara nyingi uchovu unaoleta tamaa ya chakula huonekana kwa sababu viungo vinavyoyeyusha chakula vililemewa na kazi ngumu zaidi wakati wa mchana. Baada ya kula mlo mmoja, viungo vile vinavyokiyeyusha chakula vinahitaji kupumzika. Saa tano au sita zingepita katikati ya mlo mmoja na mwingine; na watu wanaofuata utaratibu huu wataona ya kwamba milo miwili yafaa kwa siku moja kuliko mitatu. KN 253.6

Desturi ya kula milo miwili kwa siku inaonekana hasa kuwa jambo la kufaa kwa afya; lakini, wakati mwingine, huenda watu wakahitaji mlo wa tatu. Walakini, kama ukitwaliwa, yafaa uwe kidogo sana, na wa chakula ambacho huyeyushwa kwa urahisi sana tumboni. 20 KN 253.7

Wanafunzi wakiwa wanachanganya kazi za juhudi za mwili na zile za akili hakuna kizuizi cha mlo wa tatu hata kidogo, wanafunzi hao waweza kuwa na mlo wa tatu, unaotayarishwa bila kuwa na mboga za majali, bali mwepesi wenye chakula bora, kama vile matunda na mkate. 21 KN 254.1

Haifai kula chakula kilicho na moto sana wala baridi sana. Chakula kikiwa baridi sana, nguvu ya tumboni hulazimishwa kukitia chakula hicho joto kabla ya kuanza kukiyeyusha. Vinywaji vya baridi havifai kwa sababu hiyo hiyo; pia kutumia sana vinywaji ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kukiyeyusha chakula tumbom; kwa sababu ni lazima vinywaji vichujwe kwanza, ndipo kazi ya kukiyeyusha chakula ianzishwe. Usitumie chumvi nyingi sana, jiepushe na achali na vyakula vilivyokolezwa kwa kutiwa viungo vingi, tumia matunda mengi, na hamu ya maji mengi wakati ule ule wa chakula itatoweka. Yafaa chakula kiliwe pole pole, na kutafunwa kabisa. Jambo hili ni la muhimu ili mate yachanganywe vizuri na chakula, kiwe tayari kutumiwa na kuyeyusnwa na dawa za tumboni. 22 KN 254.2