Kutayarisha Njia
Matumizi ya Kanuni za Matengeneo ya Afya
Kuna busara kweli katika matengenezo ya vyakula. Yafaa somo hili kuchunguzwa sana kwa ndani, na asiwepo mtu mwenye kuwalaumu wengine kwa sababu desturi yao katika mambo yote haipatani na ile yake mwenyewe. Haiwezekani kufanya kawaida moja kusawazisha mazoea ya kila mmoja; na haifai mtu ye yote kujifikiri kuwa yu kipimo cha tabia kwa wote. Watu wote hawawezi kula vitu vya namna moja. Vyakula ambavyo ni vitamu na vizuri kwa mtu mmoja huenda vikawa vya kumchukiza, ama hata kumdhuru mwingine. Wengine hawawezi kutumia maziwa, huku wengine wakinenepeshwa nayo. Watu wengine njegere na kunde haziwezi kuwatulia tumboni; wengine huziona ni chakula bora. Kwa wengine nafaka isiyosafishwa maganda ni chakula kizuri kwao, ambapo wengine hawawezi kabisa kuzitumia. 23 KN 254.3
Wale ambao wameyaendekeza mazoea mabaya ya ulaji, inawapasa kuongoka upesi na kuyaacha mazoea yale, pasipo kukawia. Ugonjwa wa kutokiweza chakula vizuri tumboni (dyspepsia) ukisha kuingia kutokana na kulitumikisha tumbo vibaya, ni heri jitihadi ifanywe kwa uangalifu ili kuihifadhi nguvu iliyobaki katika viungo vyenye maana sana kwa uzima, kwa kuacha kila tendo linalolemea tumbo. Pengine haliwezi kupona kabisa na kuirudia hali yake ya kawaida baada ya kutumiwa vibaya kwa muda mrefu; lakini kutumia chakula kinachofaa kunaweza kuzuia udhaifu usizidi; na wengine wanaweza kupata nafuu au kupona kabisa. KN 254.4
Watu wenye nguvu ambao kila siku hufanya kazi za juhudi, haiwalazimu kujihadhari sana juu ya utamu au wingi wa chakula walacho, kama wale wafanyao kazi za kuketi; lakini hata wale wafanyao kazi za juhudi wangekuwa na afya bora kama wangezoea kujizuia katika kula na kunywa. KN 255.1
Wengine wangependa pawe na kanuni halisi juu ya chakula kinachowafaa. Hakuna mtu awaye yote awezaye kuweka kanuni halisi za chakula kwa mwingine. Ingempasa kila mtu kutumia akili zake mwenyewe na kujitawala na kufanya mambo kwa kuzishika kanuni. 24 KN 255.2
Yafaa kuzidisha ubora wa chakula kuwe jambo la kuendelea daima. Kadiri magonjwa kwenye wanyama yanavyozidi, ndivyo kutumia maziwa na mayai kutakavyozidi kuwa jambo la hatari. Yafaa jitihadi zifanywe kupata vitu vingine badala yake ambavyo ni bora kwa afya na vya bei isiyo kubwa. Yafaa watu kila mahali wafundishwe jinsi ya kupika bila kutumia maziwa wala mayai, kadiri iwezekanavyo, lakini, wawe na chakula kizuri tena kitamu. KN 255.3
Mungu hatukuzwi miili yetu isipotunzwa ama ikitumiwa vibaya, na kwa njia hiyo hufanywa isifae kwa kazi yake. Kutunza mwili kwa kuupatia chakula kilicho na ladha na chenye kutia nguvu ni mojawapo ya wajibu wa kwanza wa mwenye nyumba. Ni heri kuwa na nguo na vyombo vya bei ndogo kuliko kujihinisha chakula. KN 255.4
Wenye nyumba wengine hutoa chakula kidogo mezani mwa watu wa nyumbani mwao ili wawakaribishe wageni kwa vyakula vya bei kubwa. Hiyo si busara. Yafaa makaribisho ya wageni yawe mapesi zaidi. Mahitaji ya watu wa nyumbani hayana budi kuangaliwa kwanza. KN 255.5
Kutotumia fedha kwa uangalifu pamoja na desturi zingine za kuiga ovyo mara nyingi huzuia ukarimu unapotakikana ambapo ungekuwa mbaraka. Kiasi cha chakula kwa kawaida mezani mwetu kingekuwa cha kutosha kusudi mgeni asiyetazamiwa akifika aweze kukaribishwa bila kumtwisha mzigo mama mwenye nyumba kufanya matayarisho mengine ya chakula. KN 255.6
Fikiria juu ya chakula chako kwa uangalifu. Jifunze njia itakayoleta matokeo mema. Kuza tabia ya kujizuia. Itawale tamaa ya chakula kwa busara. Kamwe usilitumie vibaya tumbo kwa kula kupita kiasi, lakini usijinyime chakula bora na kitamu kitakiwacho kwa afya. KN 255.7
Wale ambao huzifahamu kanuni za afya na wenve kutawaliwa na kanuni, wataepukana na vyakula vya anasa na kutojihusuru pia. Chakula chao huchaguliwa, siyo kwa ajili ya kuridhishwa tamaa ya chakula, bali kwa ajili ya kuujenga mwili. Wanatafuta kuuhifadhi kila uwezo katika hali njema kabisa kwa ajili ya kazi bora sana kwa Mungu na kwa wanadamu pia. Tamaa ya chakula hutawaliwa na akili na dhamiri ya moyoni, nao hupata ijara ya afya njema ya mwili na akili. Huku wakiwa hawasisitizi vibaya maoni yao kwa wengine, kielelezo chao ni ushuhuda wa mafundisho mazuri. Watu nawa wanao mvuto mkubwa kwa mema. 25 KN 255.8
Haitupasi kutumia chakula kingi zaidi siku ya Sabato. Badala ya kufanya hivyo, chakula kingekuwa chepesi, na kingeliwa kiasi cha kutosha tu, kusudi tuwe na akili timamu yenye nguvu ya kuyafahamu mambo ya kiroho. KN 256.1
Kupika chakula siku ya Sabato kungeepukwa; lakini maana yake si kwamba hatuna budi kula chakula baridi. Katika siku za baridi chakula kilichopikwa Ijumaa kingepashwa moto. Na ulaji wote ya siku ya Sabato, ingawa niwepesi namna gani, uwe ‘mtamu na wa kupendeza. Hasa katika nyumba ambapo kuna watoto, ni jambo jema, siku ya Sabato, kutumia chakula fulani kipendwacho, ambacho watu wa nyumbani humo hawakitumii kila siku. 26 KN 256.2