Kutayarisha Njia

193/210

Elimu ya Upishi

Upishi si elimu ya kudharauliwa, na ni kazi ya muhimu zaidi katika maisha ya kila siku. Ni elimu inayompasa kila msichana kujifunza, na ingefundishwa kwa namna inayoweza kuwanufaisha watu wa aina zote. Kupika chakula kisichokolezwa kwa viungo, chenye manufaa, tena kukitengeneza kiwe kitamu, inatakikana ujuzi mwingi; lakini inawezekana. Inawapasa wapishi kujua namna ya kukitengeneza chakula chepesi kwa njia rahisi na ya afya, ili kiwe kitamu, na chenye kuitia afya, kwa jinsi kilivyotengenezwa bila kuchanganywa na viungo vingi. 4 KN 251.5

Tumnyeni maendeleo ya akili katika kukifanya chakula chetu kuwa chepesi (kisichokolezwa kwa viungo vikali) kwa majaliwa ya Mungu kila nchi hutoa vitu mbalimbali vyenye kutia afya ambavyo ni muhimu kwa kuujenga mwili. Hivi vyaweza kufanywa viwe vyakula vya kupendeza vitiavyo afya. 5 KN 251.6

Wengi hawaoni kuwa hili ni jambo liwapasalo, kwa hiyo, hawajaribu kutayarisha chakula vizuri. Hilo laweza kufanywa kwa njia nyepesi ya kutia afya, na kwa urahisi, bila kutumia shahamu, siagi, wala nyama. Akili haina budi kuchanganywa na utovu wa viungo vya chakula. Ili kufanya hivi, wanawake hawana budi kusoma, kisha kwa saburi, kuyapatanisha mambo wasomayo na kuyatumia maishani. 6 KN 251.7

Matunda, nafaka, na mboga za majani, vikitayarishwa kwa njia nyepesi bila kutiwa viungo wala shahamu yo yote, na kuchanganywa na maziwa au mafuta yanayopatikana katika maziwa yaliyochemshwa (cream) huwa chakula bora sana kwa afya. 7 KN 252.1

Nafaka na matunda bila shahamu, yakiwa na hali yake ya asili kadiri iwezekanavyo, hufaa kuwa chakula mezani mwa wote wanaodai kujitarisha kutwaliwa mbinguni. 8 KN 252.2

Sukari nyingi zaidi inatumiwa katika chakula. Keki, maandazi, sambusa, ute mzito ulio mtumu (jelly) na mraba vinakifanya chakula kisiyeyushwe kwa urahisi tumboni. Vyakula vyenye madhara zaidi ni vile vinavyotengenezwa kwa kuchanganya maziwa, sukari na mayai pamoja. Kutumia kwa wingi maziwa na sukari pamoja hakufai. 9 KN 252.3

Kadiri sukari pangufu inavyotumiwa katika kutayarisha chakula, ndivyo matata yanayotokana na joto la hali ya nchi yatakavyozidi kupungua. 10 KN 252.4

Maziwa yakitumiwa, yafaa kuchemshwa kabisa ili kuviua vijidudu vya ugonjwa; onyo hili likishikwa, hakuna hatari sana ya kupatwa na ugonjwa katika kutumia maziwa. 11 KN 252.5

Pengine utafika wakati ambapo haitakuwa salama kutumia maziwa. Lakini, ikiwa ng’ombe ni wenye afya na maziwa yakichemshwa vizuri, hailazimu kuufanya wakati huo wa shida ufike mapema zaidi kabla ya wakati wake. 12 KN 252.6

Vyakula Vilivyokolezwa Sana kwa Viungo KN 252.7

Viungo vikali vya kukoleza chakula, ambavyo mara nyingi hutumiwa na walimwengu, hudhuru kazi ya kukiyeyusha chakula tumboni. 13 KN 252.8

Katika zama hizi za ufasiki, chakula kisichochochea mwili chafaa zaidi, Kwa kawaida viungo vya kukoleza huleta madhara. Haradali, pilipili, viungo vingine vya chakula kama vile basibasi, dalasini, achali na vitu vingine vya jinsi hii, vinaunguza matumbo na kuuharakisha mwendo wa damu na kuunajisi. Hali ya kuungua inayoonekana katika matumbo ya mlevi ni kielelezo cha matokeo ya pombe. Hali ifananayo na hii inapatikana kwa kuvitumia viungo vya chakula vinavyounguza matumboni. Halafu mtu hawezi kuridhika na utamu wa chakula cha kawaida. .14 Mwili utakuwa ukihitaji na kutamani sana kitu ambacho huonekana kwamba kinautia mwili nguvu kumbe sivyo14 KN 252.9

Wengine wameiendekeza tamaa vao ya chakula, kama wasipopata chakula kile hasa wanachokitamani, hawana raha chakulani. Ikiwa viungo vikali vya chakula na vyakula vilivyokolezwa huwekwa mbele yao, hulifanya tumbo kutenda kazi kwa kutumia mchapo huo mkali; maana limetumiwa vibaya hata haliwezi tena kukubali chakula kisichochochea. 15 KN 253.1

Viungo vya chakula kwanza vinaunguza matumbo, lakini hatimaye hunaribu wepesi wa asili wa utando mweroro wa tumboni. Damu huchafuka, tamaa za kinyama huamshwa, huku nguvu za tabia ya uadilifu na za akili hudhoofishwa, na kutumikia tamaa mbaya zaidi za mwili. Yafaa mama ajifunze kuandaa chakula chepesi, kisichokolezwa kwa viungo, lakini chenye kuulisha mwili, mbele ya jamaa yake. 16 KN 253.2