Kutayarisha Njia
Mpango wa Kwanza wa Mungu kwa Chakula cha Mwanadamu
Ili kujua namna ya vyakula vilivyo bora kabisa, inatupasa kujifunza mpango wa kwanza wa Mungu juu ya chakula cha mwanadamu. Yeye aliyemwumba mwanadamu na kufahamu mahitaji yake ndiye aliyemchagulia Adamu chakula chake. Akasema, “Tazama, nimewapa kila mehe utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu.” (Mwa. 1:29). Adamu alipoondoka Edeni apate kuishi kwa kulima mashamba, baada ya kulaaniwa kwa ajili ya dhambi, aliruhusiwa kutumia pia “mboga za kondeni.” (Mwa. 3:18). KN 250.4
Nafaka, matunda, kokwa, na mboga ndivyo vyakula tulivyochaguliwa na Muumba wetu. Vyakula hivi, vikiandaliwa bila kukolezwa viungo vikali, huleta afya mwilini na kututia nguvu. Humtia mtu nguvu, uwezo wa kuishi miaka mingi, na akili timamu ambazo hazipatikani katika vyakula vilivyoungwa sana. 2 KN 251.1
Mtu akitaka kudumu kuwa na afya njema, inampasa apate chakula kizuri cha kutosha, na kinachoujenga mwili. KN 251.2
Tukipanga mambo kwa busara, vyakula vinavyoleta afya vinaweza kupatikana karibu katika kila nchi. Namna mbalimbali za mchele, ngano, mahindi na shayiri zinapelekwa pande zote, na maharagwe, mbaazi na dengu vilevile. Vyakula hivi, pamoja na matunda ya asili pamoja na yale yanayoletwa kutoka nchi nyingine, na namna nyingi za mboga zinazositawi katika kila nchi, hutuwezesha kuchagua ulaji ya namna nyingi tupendavyo bila kutumia nyama. KN 251.3
Popote yapatikanapo matunda yaliyokaushwa, kama zabibu kavu, zambarau, na matunda madogo madogo kama vile maepo, mapea, mapichi, na aprocots kwa bei ya chini, yangetumiwa kama chakula cha kawaida, kwa sababu yanafaa sana kwa afya, na yanaweza kutumiwa na watu wanaofanya kazi ya aina yo yote. 3 KN 251.4