Kutayarisha Njia

191/210

Sura Ya 40 - Chakula Tulacho

MIILI yetu hujengwa na chakula tulacho. Kila mara mwili wa mwanadamu hupoteza sehemu yake; kila kiungo kinapojimudu hutokwa na sehemu ndogo, na sehemu zile zinazotoka hurudishwa na chakula tulacho. Kila kiungo mwilini mwetu huhitaji mifupa, musuli, na neva pia zinahitaji sehemu zao. Ni kazi ya sehemu ya chakula; mifupa. Ubongo hauna budi kupata sehemu yake; ajabu sana inayobadilisha chakula kuwa damu, na kutumia damu hii kwa kuvijenga viungo mbalimbali vya mwili; lakini kazi hii inaeendelea daima, lkileta uzima na afya kwa kila neva, misuli na minofu. KN 250.1

Vyakula ambavyo yafaa kuchaguliwa kwa matumizi ni vile tu ambavyo vinahitajiwa kwa kuujenga mwili. Maana yake, si kwamba inatupasa kuchagua chakula kwa ajili ya utamu wake tu. Tamaa ya chakula ya watu wengi imepotoka kwa ajili ya desturi mbaya za kula. Mara nyingi hutamam chakula kinachodhoofisha mwili na kuleta udhaifu badala ya nguvu. Si lazima tuongozwe na desturi za kikabila. Maradhi mengi na maumivu yanayoenea pote duniani hutokana na makosa ya wanadamu katika kuchagua vyakula. KN 250.2

Lakini si kwamba vyakula vyote vilivyo na manufaa vinafaa mahitaji yetu katika hali zote. Ingetupasa kujihadhari sana katika hali zote. Ingetupasa kujihadhari sana katika kuvichagua vyakula. Chakula chetu kingefuatana na hali ya majira, hali ya nchi tunapokaa, pamoja na kazi tunayoifanva. Vyakula vingine ambavyo vinaweza kutumiwa katika majira fulani ya mwaka na katika hali fulani ya nchi havifai kutumiwa kwa hali ya nchi nyingine, na katika majira mengine. Hivyo kuna vyakula maalumu vinavyofaa kwa watu wanaofanya kazi za namna mbalimbali. Mara nyingi chakula kinachofaa kutumiwa na watu wanaofanya kazi ngumu za juhudi hakifai kutumiwa na watu wanaofanya kazi za ofisini za kuketi na kufikiri. Mungu ametupa namna mbalimbali za vyakula vyenye kuleta afya, na inampasa kila mtu achague namna ya vyakula ambavyo kwa ujuzi wake ameviona kuwa vinafaa kwa mahitaji yake. 1 KN 250.3