Kutayarisha Njia
Sura Ya 39 - Faida ya Usafi
ILI kuwa na afya njema, hatuna budi kuwa na damu nzuri; maana damu ni mkonao wa uhai. Hujenga mahali palipoharibika, na kuulisha mwili. Ikipatiwa vyakula bora kwa afya na kusafishwa pamoja na kutiwa nguvu kwa kukutana na hewa safl, hupeleka uhai na nguvu kwa kila sehemu ya mwili. Kadiri mwendo wa damu mwilini unavyokuwa kamili, ndivyo na kazi hii itakavyotimizwa vizuri. 1 KN 247.1
Kutumia maji kwa kuusafisha mwili ni njia nyepesi ya kufaa sana kuurahisisha mwendo wa damu mwilini. Kuoga maji baridi au maji ya uvuguvugu kwafaa sana kwa ajili ya kuutia mwili nguvu. Maji ya kuogea yenye joto la kadiri huvifunua vinyweleo, na hivyo husaidia kuondoa uchafu mwilini. Kuoga kwa maji ya uvuguvugu au yenye joto la kutosha hutuliza na kuburudisha neva na kuusawazisha mwendo wa damu mwilini. KN 247.2
Mazoezi ya viungo vya mwili yanatia damu nguvu na kuusawazisha mwendo wake mwilini, lakini kukaa kivivu huifanya damu, isisaflri salama, na kwa hiyo mabadiliko ndani yake, ambayo ni ya muhimu sana kwa uhai na afya ya mwili, hayafanyiki. Ngozi pia haitendi kazi yake. Uchafu hautolewi kama vile ambavyo ingalikuwa ikiwa mwendo wa damu ungeharakishwa kwa kufanya mazoezi ya juhudi, na kuitunza ngozi ya mwili iwe na hali njema ya afya, pamoja na kuvuta hewa safi kwa wingi mapafuni. 2 KN 247.3
Yafaa mapafu kuachiwa nafasi ya kutosha iwezekanavyo. Ukubwa wake hunyoshwa na kunyumbuka kwa kupumua vizuri bila mbano wo wote; hupungua yakizuiwa na kubanwa. Kwa hiyo matokeo mabaya ya kuyabana yanaonekana, hasa kwa wale wafanyao kazi za kuketi kitako, wakizoea kujikunyata wasiketi wima. Kuketi hivi ni vigumu kupumua vizuri. Hatimaye kupumua kwa juu juu huwa mazoea, na mapafu hupoteza uwezo wake wa kunyumbuka. KN 247.4
Hivi, mwili haupati ‘oxygen’ ya kutosha. Damu huzunguka mwilini pole pole. Uchafu wenye sumu ambao unafaa kutoka mapafum wakati wa kuvuta pumzi, hukawilishwa, na damu huchafuka. Kwa njia hii, licha ya mapafu, hata na tumbo, ini na ubongo pia hudhuriwa. Ngozi inakunjuka na kupoteza rangi yake; kazi ya matumbo ya kukiyeyusha chakula hukawilishwa; moyo hupunguzwa nguvu; ubongo husumbuliwa; na mafikara huchafuliwa, moyo huwa mzito, na mwili wote hudhoofika na kulegea; na hivi huwa katika hali ya kupatwa na ugonjwa kwa urahisi. KN 247.5
Mapafu huwa aaima yanajiondolea uchafu, na hiyo yanahitaji kupewa hewa safi kwa uthabiti. Hewa chafu haiwezi kutoa okisijeni inayotakiwa, na hivyo damu hupita mpaka kwenye ubongo na hata kwenye viungo vingine vya mwili bila kutiwa nguvu. Kwa sababu hiyo kupisha hewa safi kwa kweli ni kitu cha lazima. Kuishi katika vyumba vilivyofungwa, vyenye uhaba wa kuingiza hewa safi, ambapo hewa imehanbika na mbovu, kunadhoofisha mfumo wote. Mwili unakuwa mwepesi wa kuona baridi kwa njia ya peke yake, na ukikaa nje penye baridi kidogo tu unavuta magonjwa. Kujifungia ndani ya nyumba ndiko kunakofanya wanawake wengi wawe dnaifu na kugeuka rangi. Wanavuta hewa iyo hiyo wakati wote mpaka inajaa vitu vyenye sumu zilizotupwa nje kwa njia ya mapafuni na kwenye vinyeleo, na hivyo uchafu hurudishwa tena kwenye damu. 3 KN 248.1
Wengi huumia kwa ugonjwa kwa sababu hawakubali kupata hewa safi ya usiku vyumbani mwao wakati wa usiku. Hewa safi ya anga, itolewayo bure, ni mojawapo ya mibaraka mikubwa tuwezayo kuifaidi. 4 KN 248.2
Usafi kamili katika kila jambo ni lazima kwa afya ya mwili na ya rohoni. Uchafu wa kila namna huondolewa mwilini daima kwa njia ya ngozi. Vinyweleo milioni vya ngozi huzibwa upesi visiposafishwa kwa maji mara kwa mara, na hivi uchafu ambao ungepitia ngozini huwa unavizidishia kazi viungo vingine vinavyoondosha uchafu toka mwilini. KN 248.3
Watu wengi wangefaidiwa kama wangeoga kila siku kwa maji baridi au yaliyo vuguvugu, asubuhi au jioni. Badala ya kuwa na nali ya kupatwa na mafua, akifanya bidii kuoga kila siku, atazuia mafua, kwa sababu kuoga kuna rahisisha mwendo wa damu mwilini; damu hukaribiwa na ngozi, na kutiririka kwa urahisi katika mishipa yake. Ubongo na mwili pia hutiwa nguvu. Musuli zinaweza kujimudu kwa urahisi zaidi, na akili zinaamshwa. Kuoga kunaburudisha neva. Kuoga kunasaidia matumbo na ini, na kuziletea afya na nguvu sehemu hizo, na hufanya tumbo kukiweza chakula. KN 248.4
Pia ni jambo la muhimu kuwa mavazi yawe safi, Mavazi yaliyovaliwa hushika uchafu unaotoka mwilini kwa njia ya vinyweleo; na yasipobadilishwa mara kwa mara na kusafisnwa, uchafu utaingizwa mwilini tena. KN 248.5
Uchafu wa kila namna huleta ugonjwa. Vijidudu vinavyoleta kifo hujificha mahali pa giza, katika pembe za nyumba zisizofagiliwa, katika takataka zilizooza, na penye chepechepe, kutu na koga. Mboga inayotupwa, au mafungu ya majani ya miti yaliyopukutika, yasingeachwa karibu na nyumba yaoze na kuitia hewa sumu. Kitu cho cnote kilicho kichafu ama kinachooza hakina budi kuondolewa mbali na nyumba. KN 248.6
Usafi kamili mwanga wa jua, uangalifu mkuu juu ya kila kitu cha maisha ya nyumbai, haya yote ni mambo ya muhimu sana ili watu waepukane na magonjwa, na kuwa na furaha na nguvu nyumbani. KN 249.1
Wafundishe watoto kuwa Mungu hapendezwi kuwaona na miili iliyo michafu wala mavazi ya ovyo yaliyoraruka. Kuwa na mavazi safi itakuwa ndiyo njia mojawapo ya kuyaweka mafikara katika hali nzuri ya usafi. Hasa kiia kitu kinachogusana na ngozi kingewekwa safi. KN 249.2
Kamwe Kweli hakukanyaga kwa miguu yake miangalifu katika njia yenye uchafu wala unajisi. Yeye ambaye alikuwa mwangalifu sana ili kwamba wana wa Israeli wahifadhi mazoea ya usafi hataruhusu uchafu wo wote nyumbani mwa watu wake leo. Mungu huuchukia uchafu wo wote. KN 249.3
Pembe chafu, ambazo zimeachwa ovyo nyumbani bila kutunzwa, zitaelekea kufanya pembe chafu zisizoangaliwa moyoni mwa mtu. KN 249.4
Mbinguni ni mahali pasafi na patakatifu, na wale ambao hupita katika malango ya mji wa Mungu huvikwa usafi wa ndani na nje pia. 6 KN 249.5