Kutayarisha Njia
Onyesha Utengemano wa Afya
Katika kazi yetu imepasa uangalifu mkubwa kutumiwa kwa utengemano wa kuwa na kiasi. Kila kazi inayohitaji utengemano huo huleta kuongoka, imani na utii. Yaani, huinua mtu kwenye maisha mapya na yaliyo bora zaidi. Hivyo kila utengemano wa kweli una mahali pake katika kazi ya ujumbe wa malaika wa tatu. Hasa kuwa na kiasi hudai uangalifu na msaada wetu. Katika mikutano yetu ya makambi ya kila mwaka tungeangalia kazi hii na kuifanya jambo lenye nguvu. Yafaa kuwaonyesha watu kanuni za kuwa na kiasi kwa kweli na kuwaita watu kutia sahihi ahadi ya kuwa na kiasi. Uangalifu mkubwa ungetumiwa kwa wale ambao wametawaliwa kabisa na mazoea mabaya. Yatupasa kuwaongoza kwenye msalaba wa Kristo. KN 245.5
Kadiri tunavyoukaribia mwisho hatuna budi kuzidi kuinuka juu kwa jambo hili la utengemano wa afya na kuwa na kiasi cha Kikristo, tukionyesha jambo hilo kwa njia dhahiri na thabiti. Yatupasa kujitahidi daima kuwafundisha watu, siyo kwa maneno yetu tu, bali kwa vitendo vyetu pia. Maneno na matendo yakiungana yana mvuto wenye nguvu. 8 KN 246.1