Vita Kuu
Ufufuo wa Kwanza
Sauti ya Mwana wa Mungu ilipowaita watakatifu waliokuwa wamelala, dunia ilitetemeka kwa nguvu sana. Waliidkia wito wake, wakaondoka wamevikwa utukufu Aa hali ya kutokufa> wakashangilia wakisema, “Ushindi, ushindi, juu ya mauti na kuzimu! Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? (Soma 1 Kor. 15:55). Ndipo watakatifu walio hai, pamoja nao waliofufuliwa wakapaaza sauti zao kwa namna ya shangwe na furaha kuu. Miili yote iliyozikwa makaburini ikiwa na alama ya maradhi na kifo sasa ilitoka maka-burini ikiwa na afya njema na hali ya kutokufa. Watakatifu walio hai hugeuzwa mara, kufumba na kufumbua, na kuungana na wale waliofufuka, nao watamlaki Bwana wao pamoja angani. Kutakuwa kukutana kwa ajabu sana! Rafiki ambao walikuwa wametengwa kwa ajili ya kifo, sasa wataungana wasitengane tena. VK 120.1
Katika kila upande wa gari lile la wingu kulikuwa na mabawa, na chini yake kulikuwa na magurudumu yaliyo hai; na gari lilipopanda juu, magurudmu yale yafipaaza sauti na kusema, “Mtakatifu” na mabawa valipokuwa yakienda, yalipaaza sauti yakisema, “Mtakatifu,” na mafuatano ya malaika watakatifu waliozunguka lile wingu walipaaza sauti wakisema, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu wa Majeshi!” Na watakatifu waliokuwa katika lile wingu walipaaza sauti zao wakisema, “Utukufu, Alleluya!” Ndipo gari likapanda juu kwenye Mji Mtaka-tifu. Kabla ya kuingia mjini, watakatifu walipangwa katika mraba ulio kamili, na Yesu akisimama katikati Naye akawapita wote kwa urefu, watakatifu hata na malaika, tangu mabega na kwenda juu. Umbo lake la utukufu na uso wake wa kupendeza uliweza kuonwa na wote waliokuwa katika mraba ule. VK 120.2