Tumaini la Vizazi Vyote

88/307

Hakuna mtu mkuu zaidi

Yesu aliongeza kusema: “Mlikwenda jangwani kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazameni wenye kupendeza, wavaao mavazi mazuri wamo katika nyumba za wafalme.” Watu matajiri wenye kujipamba, waishio kianasa, katika fahari, hawamo katika kundi la watenda kazi wa Mungu. Makuhani na wakuu wa Wayahudi walijipamba kwa fahari kubwa; kwa mavazi ya fahari. Walitafuta kuheshimiwa na watu, kuliko kutafuta upendeleo wa Mungu. Utii wao haukumwelekea Mungu, bali ulielekea kwa wafalme wa dunia hii. TVV 119.1

Yesu aliwauliza: “Lakini mlikwenda kuona nini” Nabii . . . Huyu ndiye aliyeandikiwa. TVV 119.2

“Angalieni namtuma mtumishi wangu mbele ya uso wako. Atakayetengeneza njia mbele yako. TVV 119.3

Nawaambia, katika watu waliozaliwa na wanawake, hakuna mtu mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.” Yesu aliendelea kusema, “Walakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.” Tangazo lililotolewa kwa Zakaria kabla ya kuzaliwa kwa Yohana, malaika alisema: “Atakuwa mkuu machoni pa Bwana.” Luka 1:15. Machoni pa mbingu, ni nini kinachofanya mtu kuwa mkuu? Sicho kile kinachohesabiwa na ulimwengu. Ukuu mbele ya macho ya Mungu ni kule kuwa mnyofu. Unyofu ndio Mungu huhesabu kuwa ukuu. Mungu huheshimu upendo na usafi wa maisha. Yohana alikuwa mkuu machoni pa Mungu, alipokataa kujitukuza yeye mwenyewe, ila heshima yote akaielekeza kwa Yesu, ambaye ni yeye aliyeahidiwa. Kutokuwa na ubinafsi kwake na kufurahia na kutukuza kazi ya Yesu, kulimfanya aonekane kuwa ni kielelezo halisi cha ukuu umpasao mtu. TVV 119.4