Tumaini la Vizazi Vyote

89/307

Zaidi ya Nabii

Yohana alikuwa “Zaidi ya nabii”. Wakati manabii walikuwa wakiona mbali kuhusu kuja kwa Kristo, lakini kwa Yohana alipewa kumwona na kumkabidhi kwa Israel; kama mtu aliyetumwa na Mungu. Yohana alikuwa nuru ndogo ambaye atafuatwa na nuru kuu. Hakuna nuru kuu zaidi itakayomulikia wanadamu kuliko nuru ya Yesu. TVV 119.5

Mbali na furaha Yohana aliyokuwa nayo katika kazi yake, lakini maisha yake yamekuwa yenye masikitiko kabisa. Alikuwa mtu wa huzuni, akikaa katika hali ya upweke. wala hakuweza kuishi na kuona matokeo ya kazi yake. Hakuwa na nafasi ya kuishi pamoja na Kristo, na kusikia maneno yake, ambayo ni nuru halisi, yenye kung’aa katika unabii. TVV 120.1

Herode aliamini kuwa Yohana ni nabii wa Mungu, naye alikusudia kumfungulia. Lakini alimwogopa Herodias. Alijua kuwa asipochukua hatua thabiti hawezi kumwua Yohana, ambaye anamchukia, kwa hiyo alitaka kukamilisha kusudi lake kwa njia ya hila. Siku ya kuzaliwa kwa mfalme ilifanywa sikukuu, na ulevi wa kila namna. Herode angesifiwa na kutukuzwa kama apendavyo. TVV 120.2

Sikukuu ilipofika, mfalme na wakuu wake walifanya anasa na kulewa. Herodias akamtuma bintiye katika jumba la sikukuu ili akawatumbuize wageni kwa nyimbo na michezo. Binti wa Herodias ambaye ni Salome, alikuwa katika kilele cha ujana wake. Akacheza kwa madaha na maringo sana, akawapendeza na kuwafurahisha wakuu wote. Wakamsifu Herode na kumtukuza kwa ajili yake. TVV 120.3

Mfalme alikuwa amelewa kwa mvinyo. Akapumbaa. Hakuweza kufikri kitu zaidi, ila karamu, jumba la karamu, mvinyo, taa na msichana akicheza mbele yao. Wakati ule bila kufikiri sawa, alitaka kutenda kitu kitakachomletea fahari na kutukuka zaidi mbele ya wakuu wake, walioko kwenye karamu hiyo. Alitoa ahadi kwa binti huyo wa Herodias kwamba aombe kitu chochote atapewa, hata nusu ya ufalme wake. TVV 120.4

Salome akakimbia kwa mama yake, na kumwuliza kuwa aombe kitu gani? Jawabu lilikuwa tayari, kichwa cha Yohana Mbatizaji. Salome alisita kuomba kitu hicho, lakini sisitizo la Herodias lilifaulu. Binti alirudi na haja ya kutisha. “Nataka unipe kichwa cha Yohana Mbatizaji katika sahani, sasa hivi.” TVV 120.5

Herode alishangaa na kuchanganyikiwa. Aliogopa na kushangaa kukata kichwa cha Yohana Walakini hakupenda kuonekana kuwa mwongo na, mfedhuli. Ameapa mbele ya wageni wake, na kama mtu mmoja katika wageni angelipinga jambo hilo, Herode angefurahi kumwacha hai nabii. TVV 120.6

Aliwapa nafasi kuzungumza kuhusu Yohana, ambaye ni mfungwa. Walifahamu kwamba Yohana ni mjumbe wa Mungu. Lakini waliogopa kwa ajili ya matakwa ya msichana, na kwa kulewa kwingi hawakuweza kutoa shauri lolote. Hakuna mtu aliyesema neno la kumponya mjumbe wa mbinguni. Kwa watu hawa wenye madaraka makubwa wajibu mkubwa ulikuwa juu yao, walakini walijitolea kulewa tu. Vichwa vyao vilikuwa na kizunguzungu kwa ajili ya kelele za michezo. Kwa ajili ya ukimya wao, walikubali nabii wa Mungu auawe ili kutimiza matakwa ya mwanamke mwasherati. TVV 120.7

Herode alisita kuamuru kumkata kichwa nabii. Baadaye kichwa cha Yohana kililetwa katika sahani. Sauti hiyo ya Yohana haitasikika tena ikiwaita watu watubu. Karamu ya siku moja tu iligharimu kichwa cha mtu mkuu sana, ambaye ni nabii. TVV 121.1

Mara nyingi watu watawa wasiokuwa na kosa wameangamizwa na walevi ambao wangalikuwa wahifadhi wao, kwa kutetea haki Yeye awekaye kileo kinywani mwake ajitia katika hatia ya kudhulumu chochote katika uwezo wake. Wale walio waamuzi katika mambo ya maisha ya wengine, watakuwa hatia wanapojitolea kuwa walevi. Wanahitaji kuwa watu wenye mawazo kamili, afya kamili, na unyofu kamili, ili wawe na hali kamili ya kutenda mambo ya haki. TVV 121.2

Herodias alifurahia mauaji hayo ya kikatili, hali akizidi kujidai kuwa Herode atatulia, bila kuwa na wasiwasi. Lakiri matokeo yake hayatakuwa na utulivu. Jina lake lilikuwa shutuma kuu, wakati Herode alipokuwa akihangaishwa na dhamiri yake. Kila mara alikuwa akitafuta utulivu wa dhamiri. Herode hakuweza kuwa na utulivu, alipokumbuka jinsi Yohana alivyokuwa mtu mtawa, mwenye kujikana nafsi, maonyo yake ya kweli na mashauri yake safi. Alionekana kana kwamba anachangamka, lakini kwa ndani alikuwa mwenye taabu.. Alikuwa na hakika kuwa Mungu aliona mambo ya karamu yake, akaona maazimio ya Herodias, na kukiona kichwa cha Yohana, ambaye alikuwa mwonyaji wake. TVV 121.3

Herode alipoisikia kazi ya Kristo, alidhani kuwa Mungu amemfufua Yohana kutoka ufuni. Alihofu na kufikiri kuwa Yohana atalipa kisasi kwa kumwadhibu yeye na nyumba yake. Herode alikuwa akivuna mavuno ya dhambi zake; yaani kuwa na wasiwasi moyoni, kupofuka macho, na kutetemeka daima moyoni mwake. Asubuhi itasema: “Heri jioni, na jioni utasema, Heri asubuhi, kwa ajli ya hofu ya moyo wako.” Torati 28:65-67. Hakuna masumbuko makuu kuliko kuwa na wasiwasi moyoni, ambayo hakuna kupumzika mchana wala usiku. TVV 121.4