Tumaini la Vizazi Vyote

87/307

Yesu atoa vithibitisho

Siku iliendelea kumalizika, na wanafunzi wa Yohana waliona na kusikia mambo yote. Halafu Yesu aliwataka wanafunzi hao wa Yohana, akawaambia waende wamweleza Yohana yote waliyoona na kusikia. Akaongeza kusema: “Heri mtu yule asiyechukizwa nami.” Uthibitisho wa Mungu wake ulikuwa umeonekana wazi, utukufu wake ulionekana dhahiri hata kwetu sisi watu wa hali ya chini. TVV 118.1

Wanafunzi walichukua ujumbe huo, ikatosha. Yohana akakumbuka unabii uliomhusu Masihi. “Bwana amenitia mafuta, niwahubiri wanyenyekevu habari njema. Amenituma niwagange waliovunjika moyo, kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.” Isaya 6:1. Kazi ya Kristo ilijidhihirisha kuwa yeye ni Masihi. Yesu alifanya kazi yake, si kama mwenye kupindua wafalme, isipokuwa kusema na watu kuhusu uzima wa milele, kwa njia ya fadhili na kujinyima. TVV 118.2

Kanuni ya maisha ya Yohana Mbatizaji ilikuwa ndiyo kanuni ya ufalme wa Masihi. Lakini kile kilichomthibitishia Kristo Uungu wake sicho ambacho kingekuwa thibitisho kwa Viongozi wa Israeli. Yohana aliona kuwa matokeo ya kazi ya Mwokozi yalikuwa chuki na malaumu. Yohana kama mtangulizi wa Kristo alikuwa akinywea kikombe kichungu ambacho Kristo mwenyewe atakinywea baadaye. TVV 118.3

Maonyo ya Mwokozi ya upole hayakuwa ya bure kwa Yohana. Ufahamu kamili kwamba ndiye Masihi ulimfanya Yohana kujitoa kamili kwa Mungu kufa na kupona, na kufanya kazi yake kamili. TVV 118.4

Moyo wa Mwokozi ulinihurumia mtumishi mwaminifu akiwamo gerezani kwa Herode. Hakutaka watu wadhani kuwa, Mungu amemsahau, au kwamba amekata tamaa na kuacha imani yake, wakati wa majaribu. Yesu alisema, “Mlikwenda jangwani kuona nini? Majani yakitikiswa na upepo?” TVV 118.5

Marabi wakiwa kama majani marefu kando ya mto wa Yordani, walisimama wakipeperushwa huku na huko katika mawazo ya watu wenye kutangatanga. Lakini kwa kuwaogopa watu waliogopa kuikanusha kazi ya Kristo, waziwazi. Lakini mjumbe wa Mungu hakuwa na roho ya woga jinsi hiyo, Yohana alinena ukweli wa namna moja kwa Mafarisayo, Masadukayo, mfalme Herode, wakuu wote, watoza ushuru na wakulima. Hakuwa kama majani yaliyokuwa yakitikiswa na upepo. Alikuwa mwaminifu kwa Mungu hata ndani ya gereza. Alikuwa na kanuni thabiti kama mwamba. TVV 118.6