Tumaini la Vizazi Vyote

56/307

Yohana awaelekeza wanafunzi wake kwa Yesu

Siku ya pili yake, wanafunzi wawili wa Yohana walipokuwa karibu naye, Alimwona Yesu tena. Mara tena uso wake uliwaka, kwa nuru ya mbinguni, alipopaza sauti yake na kusema: “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu, wanafunzi wake hawakufahamu sawasawa maana ya jina hilo Yohana analomwita, “Mwana Kondoo wa Mungu ni nini?” TVV 69.6

Walipomwacha Yohana walikwenda kumtafuta Yesu. Mmojawapo alikuwa Andrea, nduguye Simoni; mwingine alikuwa Yohana mwinjilisti. Watu hawa ndio walikuwa wanafunzi wa Yesu wa kwanza. Walimfuata Yesu wakiwa na hamu ya kusema naye, walakini wakiogopa, wakanyamaza tu, hayo yakabaki mawazoni. Je huyu ndiye Masihi? Yesu alifahamu kuwa watu wawili hawa walikuwa wakimfuata. Wao ndio walikuwa matunda yake ya kwanza katika kazi yake. Walakini akiwageukia, aliwauliza: “Mnatafuta nini?” Wakasema “Rabi, (Maana yake mwalimu) . . . unakaa wapi?” Kwa mazungumzo mafupi wakiwa hapo njiani, waliridhika kabisa. Walitamani kuishi na Yesu, na kusikia maneno yake. TVV 69.7

“Aliwaambia, njooni, mwone, Walikuja, wakaona anapoishi, wakakaa naye siku hiyo.” TVV 70.1

Kama Yohana na Andrea wangalikuwa na mioyo isiyoamini, kama walivyokuwa makuhani na wakuu, wasingalikuwa wanafunzi, bali wangalikuwa wapimaji wa kuhukumu maneno yake. Lakini kwa kuwa walitikia mwito wa Roho kwa njia ya mahubiri ya Yohana Mbatizaji sasa walimfahamu mwalimu wa mbinguni. Kwao, maneno ya Yesu yalikuwa dhahiri na mapya. Nuru ya mbinguni uliangaza katika Agano la Kale na kuwaelimisha maneno yake. Ukweli ukadhihika nuruni. TVV 70.2

Mwanafunzi Yohana alikuwa na juhudi na upendo wa halisi, na mwalimu mwenye kutafakari sana mambo. Alikuwa ameanza kupambanua “utukufu wa Mwana wa pekee wa Baba, amejaa neema na kweli.” Yoh. 1:14. TVV 70.3

Andrea alitaka kushirikisha furaha iliyomjaa. Alipokwenda kumtafuta nduguye, alisema, “Tumemwona Masihi.” Simoni pia alikuwa amesikia mahubiri ya Yohana mbatizaji, na kwa hiyo akaharakisha kwenda kwa Mwokozi. Macho ya Kristo yalisoma tabia yake na maisha yake. Haraka haraka yake, upendo wake, na fadhili zake, hali yake ya kimbelembele na ya kujitegemea; anguko lake, na kazi yake na kifo chake cha kusulubishwa. Mwokozi alisoma hayo yote. Ndipo alisema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yona, utaitwa Kefa, maana yake jiwe” TVV 70.4

Siku ya pili yake . . . Yesu . . . allmfuata Filipo, akamwambia, ‘Nifuate Filipo alitii amri hiyo mara moja, naye akawa mmojawapo wa wafuasi wa Kristo.”Filipo akamwita Nathanieli, aliyekuwa katika mkutano, wakati Yohana Mbatizaji alipomwonyesha Yesu kuwa ndiye Mwana Kondoo wa Mungu. Nathanaeli alipomwangalia Yesu, alikata tamaa. Je, mtu huyu aonekanaye kuwa mtu fukara na mwenye wasiwasi, aweza kuwa ndiye Masihi? Walakini ujumbe wa Yohana ulikuwa umemwaminisha Nathanaeli. TVV 70.5