Tumaini la Vizazi Vyote

55/307

Sura ya Kristo Haikupambanuliwa

Huyu ndiye alikuwa Kristo? Watu walimtazama kwa mshangao mkubwa aliyekuwa akisemwa kuwa ndiye Mwana wa Mungu. Walikuwa wameshangazwa sana kwa maneno ya Yohana. Alikuwa amesema kwa jina la Mungu. Walikuwa wakimsikiliza siku kwa siku, kadiri alivyokuwa akikemea dhambi zao. Na uhakika wa maneno yake kama mtu aliyetumwa na mbingu aliwatia nguvu. Lakini ni nani huyu ambaye ni mkuu kuliko Yohana? Katika kuonekana kwake na sura yake hakuna kitu cha kuonyesha ukuu wake. Kwa kweli alikuwa mtu wa kawaida tu, akivaa nguo za kawaida tu za hali ya mtu maskini. TVV 68.4

Wengine katika mkutano walikuwako katika ubatizo wa Kristo, na walisikia sauti ya Mungu. Lakini sura ya Mwokozi ilikuwa amebadilika sana. Wakati wa ubatizo wake walimwona aking’aa kwa nuru ya mbinguni, sasa amechoka na kudhoofika, anatambuliwa na Yohana peke yake. TVV 69.1

Lakini watu waliona uso ambao ulikuwa na fadhili za Uungu na mchanganyiko wa uwezo. Kila hali yake sasa ilikuwa ya kibinadamu kamili, na usemi wa upendo. Aliwashangaza watu kwa uwezo uliofichika, lakini ukionekana kidogo. Je, huyu ndiye yule ambaye amekuwa akingojewa na Waisraeli? TVV 69.2

Yesu alikuja katika hali ya kimaskini na katika hali ya unyenyekevu, ili apate kuwa kielelezo chetu na Mwokozi wetu. Kama angeonekana katika hali ya kifahari, angefundishaje unyenyekevu? je, kama Yesu angalikuja katika hali ya kifalme, yenye fahari, watu wanyonge na maskini wangepata wapi matumaini? TVV 69.3

Lakini kwa watu wengi ilionekana kuwa mtu aliyetukuzwa hivi na Yohana, haiwezekani kuwa hafifu kama sisi tulivyo. Wengi waliona uchungu, na kutatanika. TVV 69.4

Maneno yaliyotamaniwa ya kutamkwa na Yesu kuhusu kusimamishwa kwa ufalme, hayakutamkwa. Kama angalikuwa mtu wa fahari, makuhani na walimu wa Kiyahudi na wakuu wengine wangalikuwa tayari kumpokea. Lakini, mtu atakaye kusimamisha ufalme wa haki katika mioyo yao, wasingalimpokea. TVV 69.5