Tumaini la Vizazi Vyote

38/307

Isaya afafanua maneno

Mafafanuzi ya Isaya kuhusu ufalme wa Masihi, ndiyo yalikuwa majifunzo yake aliyokuwa akichunguza mchana na usiku. Soma Isaya 11:4; 32:2; 62:4. Moyo wa mtu aliyekaa katika hali ya upweke, uliyafurahia sana mafundisho ya ufunuo wa utukufu ujao. Alimtazama Mfalme katika uzuri wake, naye alijisahau mwenyewe. Aliuangalia utukufu wa utakatifu, naye alijiona kutofaa kitu. Alikuwa tayari kwenda kama mjumbe wa mbinguni na asiyefaa machoni pa mbingu. Aliweza kusimama mbele ya wafalme wa duniani bila hofu, kwa sababu ametumwa na Mfalme Mkuu. Mfalme wa wafalme. TVV 49.4

Yohana hakufahamu kamili aina ya ufalme wa Masihi, lakini alitumaini kuwa atasimamisha ufalme wa haki kulikofanya taifa la Israeli kuwa taifa takatifu. TVV 50.1

Aliwaona watu wake wakiridhika, na wakilala katika dhambi zao. Ujumbe aliopewa na Mungu ulipaswa kuwaamsha na kuwafanya kutaharuki. Kabla mbegu ya Injili haijapandwa kwao, lazima kwanza mioyo yao kulainishwa. Kabla ya kutafuta dawa ya kuponya kwa Yesu, lazima kwanza waamshwe na kuona hatari inayowakabili kutokana na majeraha ya dhambi. TVV 50.2

Mungu hatumi wajumbe wake kupeleka ujumbe kwa watu, ili kuwatumbuiza, na kuwatuliza, wakae asiwasi, bali huwaonveshei utisho wa kuzidi kuishi dhambini. Malaika hudhihirisha adhabu za Mungu wazi, ili kuwafanya watu waone haja ya kutubu na kuepuka adhabu hizo. Kisha mkono ule uliotubisha watu, hutuliza tena. TVV 50.3