Tumaini la Vizazi Vyote

39/307

Ukingoni mwa Mapinduzi

Wakati huduma ya Yohana ilianza taifa la Israeli lilikuwa ukingoni mwa mapinduzi, yaani uasi mkuu. Arkelao mfalme, alipoondolewa, Uyahudi ilikuwa imewekwa katika utawala wa Kirumi moja kwa moja. TVV 50.4

Udhalimu wa watawala wa Kirumi, na juhudi zao za kutaka kuingiza desturi za kishenzi katika Israel zilichochea chuki kubwa sana, iliyokuwa imenyamazishwa kwa njia ya kumwaga damu nyingi ya mashujaa wa Israeli. TVV 50.5

Katika hali ya mvurugano na mashindano hayo, sauti ilisikika jangwani, ambayo ni kali, ya kushtusha, lakini imejaa tumaini, ikisema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Sauti hiyo ilistua watu, maana ilikuwa na uwezo mpya. Hili lilikuwa tangazo kwamba, kuja kwa Kristo kumekaribia. Yohana alikemea dhambi kwa uwezo wa nguvu za Eliya. Maneno yake yalikuwa dhahiri, yenye nguvu. Taifa lilitaharuki. Makundi ya watu walifurika kwenda jangwani. TVV 50.6

Yohana aliwaita watu watubu. Waliwabatiza katika maji ya mto wa Yordani, kama dalili ya nje ya kutubu dhambi. Alisema kuwa watu wanaojiita kuwa wana wa Mungu, wana dhambi. Wasipotakaswa mioyoni mwao, hawatakuwa na sehemu katika ufalme wa Masihi. TVV 50.7

Wakuu, askari, walimu wa Kiyahudi, watoza ushuru, na wakulima wote walikuja kumsikia nabii. Watu wengi walitubu na kubatizwa ili wapate kushiriki katika ufalme, na sasa siri za maovu yao zimefunuliwa. Lakini Yohana aliona kuwa watu wengi hawakuwa na maungamo ya kweli, bali walikuwa nusunusu. Walijipendekeza kwa nabii, ili washiriki katika ufalme wa Masihi. Na kwa kubatizwa kwao walidumu dhambini, huku wakiheshimiwa na watu. TVV 50.8