Tumaini la Vizazi Vyote

37/307

Elimu ya Yohana isiyo ya kawaida

Kwa kawaida mwana wa Zakaria angalipata elimu yake katika shule za walimu wa Kiyahudi yaani walimu wa kawaida wa Israeli. Lakini kwa vile elimu hiyo isingaifaa katika kazi atakayofanya, Mungu alimpeleka jangwani, ili apate kujifunza kazi ya Mungu ya uumbaji. TVV 48.5

Yohana aliishi katika hali ya upweke katika vilima na vichaka na mapango, na miamba. Katika hali hii, alijiendeleza katika mazingira ya kawaida tu na ya kujinyima. Hapa ndipo angejifunza somo la viumbe na mafunuo, pamoja na mambo ya riziki. ‘Tangu utoto wake alielekezwa juu ya kazi yake na wazazi wake waaminifu. Naye alikubaliana na maelekezo hayo. Maisha ya jangwani katika hali ya upweke, yalimtenga mbali na jamii ya watu, ambako kuna ufedhuli na machafuko ya kila hali. Alikaa mbali na mashindano ya mivuto ya dhambi. TVV 48.6

Lakini maisha ya Yohana hayakuwa ya kujitesa na kujinyima mambo ya lazima. Kila mara alikuwa katika makundi ya watu wengine, na kuona mambo yanavyoendelea ulimwenguni. Akifunzwa na Roho Mtakatifu alichungua maisha ya watu, ili ajue jinsi ya kuwafikia, na kuwapa ujumbe wa mbinguni. Mzigo wa kazi yake ulikuwa juu yake daima. Kwa njia ya maombi sana, alijitia kazini kamili. TVV 49.1

Ingawa aliishi jangwani hakujiepusha na majaribu. Mwovu Shetani alimshambulia kwa majaribu ya kila nanma pia. Lakini hali yake ilikuwa safi tu. Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu aliweza kung’amua na kushinda hila za Shetani. TVV 49.2

Yohana alifungwa na kujazwa na kuwako kwa Mungu, kama Musa alivyokuwa katika milima ya Midiani. Katika makao yake ya upweke jangwani, na giza la mwituni, Yohana aliweza kuona hali ya maisha ya Waisraeli dhahiri. Shamba la Bwana la mzabibu limeharibika kabisa. Lakini hali hiyo ya matatizo, ahadi ya Mungu kama upindi wa mvua hutia tumaini. Akiwa peke yake katika giza la usiku, alisoma na kujikumbusha ahadi ya Mungu na Ibrahim, kwamba uzao wake utakuwa mwingi kama nyota za mbinguni. Mapambazuko ya asubuhi yalimwambia kuwa; ni nani atakayekuwa kama “mapamazuko ya asubuhi, wakati jua lichomozapo, na asubuhi bila mawingu.” 2 Samweli 24:4. Na katika mng’ao wa mchana aliona utukufu wakati “utukufu wa Bwana utakapofunuliwa na wenye mwili wote watakapouona pamoja.” Isaya 40:5. Kwa kicho na unyenyekevu alichunguza katika maandiko ya unabii kuhusu kuja kwa Masihi. Shilo ataonekana kabla mfalme hajakoma kutawala katika kiti cha enzi cha Daudi. Sasa wakati umefika. Mtawala wa Kirumi amekaa katika jumba la kifalme katika mlima wa Sayuni. Kwa neno la hakika la Bwana, Kristo alikuwa amezaliwa. TVV 49.3