Tumaini la Vizazi Vyote

186/307

Mtu aliyezaliwa akiwa kipofu

Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu aliyezaliwa akiwa kipofu. Wanafunzi wake walimwuliza: ‘Bwana, ni nani aliyetenda dhambi hata huyu akazaliwa akiwa kipofu, ni yeye au ni wazazi wake?’ Yesu akajibu: “Mtu huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake, lakini kazi za Mungu zipate kuonekana ndani yake .... Aliposema hivi, alitema mate udongoni, akafanya tope, akampaka kipofu machoni, akamwambia, “Nenda ukanawe katika dimbwi la Siloam (tafsiri yake’ aliyetumwa). Akaenda, akanawa akapata kuona.” TVV 267.2

Wayahudi walikuwa wakiamini kuwa, dhambi huadhibishwa katika maisha. Shetani ambaye ndiye asili ya dhambi amewaaminisha watu kuwa magonjwa na kifo ni adhabu ya Mungu anayowaadhibu watu. Mtu yeyote apatapo mambo haya huangaliwa kuwa kama mwenye dhambi mkuu. Hivyo njia iliandaliwa kwa Wayahudi ili kumkataa Yesu. TVV 267.3

“Aliyechukua maafa yetu na kuchukua huzuni zote” aliangaliwa na Wayahudi kama aliyepigwa na Mungu na kuteswa, nao walimfichia nyuso zao.” Isaya 53:4, 5. TVV 267.4

Imani ya Wayahudi juu ya jambo hili ilishikwa pia na wanafunzi wa Yesu. Baada ya kumpaka tope la macho, Yesu alimpeleka kipofu kunawa dimbwini, na macho yake yakaona. Basi Yesu alilijibu swali la wanafunzi wake kwa njia ya tendo. Wanafunzi hawakushughulika na jambo la ni nani aliyetenda dhambi, au hakutenda; ila walifahamu rehema za Mungu kwa kuponya kipofu. Hapakuwa na dawa katika dimbwi alilokwenda kipofu huyu kunawa, ila dawa ilikuwa ndani ya Kristo. TVV 267.5