Tumaini la Vizazi Vyote

187/307

Muujiza siku ya sabato

Wayahudi walishangaa na kuchukizwa kwa kuponywa, ambako ni mwujiza uliofanyika siku ya Sabato. TVV 267.6

Majirani walipomwona yule aliyekuwa kipofu akiona, waliingia shaka, maana alionekana kana kwamba ni mtu mwingine kabisa. Uso wake ulikuwa unang’aa wengine walisema: “Ndiye,” wengine walisema “Amefanana naye.” Lakini yeye alimaliza mambo kwa kusema kuwa ni yeye. Aliwasimulia habari za Yesu na jinsi alivyopony wa. Ndipo walimwuliza “Wapi aliko sasa? Alisema, “Sijui.” TVV 267.7

Katika baraza la Wayahudi, aliulizwa jinsi alivyoponywa. Aliwaambia: “Alifanya tope akanipaka machoni, nikanawa, na sasa naona. Mafarisayo walisema kuwa, huyu si mtu wa Mungu, kwa kuwa haitunzi Sabato. Mafarisayo walikazania utunzaji wa Sabato, na hali walikuwa wanapanga kuua mtu siku ya Sabato. Lakini watu wengi walisadiki kuwa aliyemponya kipofu ana uwezo zaidi ya binadamu. Walisema: “Mtu mwenye dhambi anaweza kufanya mwujiza?” TVV 268.1

Mara tena Marabi walimwuliza kipofu: “Wewe wasemaje juu ya mtu huyu, aliyekuponya? Akasema: ‘Ni nabii.” Mafarisayo wakasema kuwa, hakuzaliwa akiwa kipofu. Wakawaita wazazi wake wakasema: “Je, huyu ni mwana wenu msemaye kuwa alizaliwa kipofu?” TVV 268.2

Mtu mwenyewe yuko anayeeleza kuwa alizaliwa kipofu na sasa anaona. Mafarisayo waliona kuwa ni heri kukataa ushuhuda wake, kuliko kukubali kosa lao. Walishikilia ukaidi wao, na kujitumainia kuwa wao, Mafarisayo ni wenye haki kamili. Mafarisayo walikuwa na tumaini moja limebaki. Nalo ni kuwatisha wazazi wa mtu huyo waseme mengine. Waliuliza: “Sasa anaona kwa vipi?” Maana ilikuwa imetangazwa kwamba, mtu atakayemkiri Yesu kuwa ni Masihi, atatengwa mbali na ushirika, yaani atatengwa kwa siku thelathini. Hukumu hiyo ilihesabiwa kuwa ni msiba mkubwa, jambo kubwa alilotendewa mwana wao, liliwaaminisha, lakini kwa ajili ya hofu walisema: “Tunajua kuwa huyu ni mwana wetu, na alizaliwa kipofu, walakini jinsi alivyopata kuona hatujui. Yeye ni mtu mkubwa, mwulizeni yeye mwenyewe.” Walitupa mambo yote kwa mwana wao. TVV 268.3