Tumaini la Vizazi Vyote

185/307

Yesu hakuwa na dhambi

“Nani anishuhudiaye kuwa nina dhambi” Ninaposema kweli mbona hamwamini?” Kwa muda wa miaka mitatu maadui wa Kristo walitafuta kasoro kwa Yesu wala hawakupata. Shetani alikuwa akitafuta njia ya kumshinda, lakini hakuweza kupata chochote juu yake cha kumshika. Hata mashetani pia walilazimika kuungama na kusema: ‘“Wewe ni mtakatifu wa Mungu.” Marko 1:24. Yesu aliishi akishika sheria mbele ya mbingu, na mbele ya viumbe ambavyo havikuanguka dhambini, na mbele ya binadamu wenye dhambi. Alinena maneno yasiyokanushika na mtu yeyote, ‘Siku zote natenda mambo yapendazayo mbele za Mungu.’” TVV 265.5

Wayahudi hawakuitambua sauti ya Mungu ndani ya Mwana wake. Walijidhani kumhukumu, lakini waukuwa wakijihukumu wenyewe. Yesu alisema: “Aliye wa Mungu husikia sauti ya Mungu, ninyi basi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.” TVV 265.6

Wengi wanaotaka kulaghai, kulaumu, na kudadisidadisi neno la Mungu hudhani kuwa hiyo ndiyo njia ya maendeleo na ufasaha. Lakini ni kujidhuru na kusaliti njia ya Ukristo. Kama vile maua huelekea kwenye jua ili lipate kurembeshwa, hali kadhalika moyo wa mtu wapaswa kuelekea kwa jua la haki ili kurembesha tabia; kwa neema ya Kristo. TVV 266.1

Yesu aliendelea kusema: “Baba yenu Ibrahim alishangilia kuona siku yangu, akaiona na kufurahi.” Ibrahim aliomba kabla ya kufa kwake amwone Masihi. Alipewa ufahamu wa pekee. Alifahamishwa kuhusu kufa kwa Mwenyezi kwa ajili ya dhambi. Kwa jambo hili alifanya kielelezo chake mwenyewe. Aliagizwa: “Umchukue sasa mwana wako Isaka, umpendaye . . . ukamtoe sadaka ya kuteketezwa.” Mwanzo 22:2. Juu ya madhabahu alimweka mwana wa ahadi, kisha akiinua kisu chake kumchinja, ili kumtii Mungu, alisikia sauti ya Mungu kutoka mbinguni ikisema: “Usimchinje mwanao, kwani sasa najua kuwa unamcha Mungu, ukiwa hukumzuilia mwanao Isaka, mwana wa pekee.” Mwanzo 22:2,12. Amri kali hii ilitolewa kwa Ibrahim ili apate kuiona siku ya Kristo, na kutambua upendo wa Mungu kwa ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili apate kuuokoa. TVV 266.2

Kwa kujitoa kikamilifu kwa Mungu, Ibrahim alionyesha kuwa kwa ajili ya kutoa Mwana wake wa pekee ili kuuokoa ulimwengu, Mungu alikuwa akitoa kipawa cha ajabu ambacho mtu hajawahi kutoa. TVV 266.3

Katika kipawa cha Mungu badala ya Isaka, ilitangazwa kwamba hakuna mtu awezaye kujitolea, kafara ili ajiokoe. Kafara za watu wa mataifa wanazotoa ili kujifaidia, hazikubaliki mbele za Mungu. Hakuna mtu awezaye kumtoa mtoto wake awe kafara. Mwana wa Mungu peke yake ndiye awezaye kubeba dhambi zote za ulimwengu. TVV 266.4

Maneno ya Kristo kuhusu Ibrahim hayakuwapa wasikilizaji wake maana kubwa zaidi. Mafarisayo waliona tu ni mambo ya utani. Waliendelea na hali yao tu ya kuona kuwa Yesu ana wazimu. Maana walisema: ‘Hujapata bado hata miaka hamsini, nawe umemwona lbrahitnu?’ Yesu alijibu kwa fahari: “Amin, amin nawaambieni kabla Ibrahim hajakuwapo, mimi nipo.” Mkutano wote ukawa kimya. Jina la Mungu lililopewa Musa ili alitangaze, mtu huyu Rabi wa Galilaya anajitia kuwa ni yeye. Amejitangaza kuwa yeye ni wa milele kama Mungu, ambaye “matokeo yake yamekuwa tangu milele.” Mika 5:2. TVV 266.5

Makuhani na wakuu wakampigia kelele Yesu kwa kuwa anakufuru, maana anajitukuza mwenyewe. Watu wengi waliungana na makuhani na marabi wakachukua mawe ili kumpiga. Lakini Yesu akajificha akatoka hekaluni. TVV 267.1