Tumaini la Vizazi Vyote

184/307

Swali kuhusu kurithi Utume

Jinsi uzao wa Ibrahim ulivyojulikana, si kwa majina tu ila kwa mfanano wa hali kadhalika kwa mitume, sio kwa vyeo na madaraka, ila kwa mfanano wa tabia na hali ya maisha ya kiroho. Maisha ya kiroho waliyokuwa nayo mitume na mafundisho waliyofundisha, ndiyo ushahidi kuwa mfanano wa mitume. TVV 265.2

Yesu alisema: “Kazi ya baba yenu ndiyo mfanyayo.’ Kwa dhihaka Wayahudi walijibu ‘Hatukuzaliwa kwa zinaa, tunaye Baba mmoja ndiye Mungu.” Maneno haya yalitajwa ili kuwafanya watu waliomwamini Kristo wababaike. Yesu hakuyajali hayo, bali alisema: “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda maana nilitoka kwake” TVV 265.3

Yesu akasema: ‘Ninyi ni wa baba yenu Shetani”, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kufanya. Alikuwa mwuuaji tangu mwanzo, naye hakuwa katika kweli hata kidogo, maana hakuna kweli ndani yake . . . Nisemapo kweli mbona hamwezi kuniamini?’ Ukweli ni kwamba Yesu alikuwa akinena kweli hasa ndiyo sababu waongozi wa Wayahudi hawakumtaka. Ukweli uliwafunua na kudhihirisha makosa yao, hivyo hawakuutaka. Wao hawakuipenda kweli. TVV 265.4