Tangu Sasa Hata Milele
Kutafuta Amani
Mapenzi ya kupata amani pamoja na Mungu yakamwongoza kujitoa mwenyewe kwa maisha ya utawa. Hapa alikuwa akitakiwa kufanya kazi ngumu za chini sana na kuomba omba nyumba kwa nyumba. Akaendelea kwa uvumilivu katika kujishusha huku,akiamini hii kuwa lazima sababu ya zambi zake. TSHM 53.2
Alijizuia mwenyewe saa zake za usingizi na kujinyima hata wakati mdogo wakula chakula chake kichache, akapendezwa na kujifunza Neno la Mungu. Alikuta Biblia iliyofungiwa mnyororo kwa ukuta wa nyumba ya watawa, na kwa hiki (Biblia) akaenda mara kwa mara. TSHM 53.3
Akaanza maisha magumu sana zaidi, akijaribu kufunga,kukesha, na kujitesa kwa kutisha maovu ya tabia yake. Akasema baadaye, “Kama mtawa angeweza kupata mbingu kwa kazi zake za utawa, hakika ningepaswa kustahili mbingu kwa kazi hiyo. ... Kama ingeendelea wakati mrefu, ningepaswa kuchukua uchungu wangu hata kufa.” Kwa bidii yake yote, roho ya taabu yake haikupata usaada. Mwishowe akafika karibu hatua ya kukata tamaa. TSHM 53.4
Wakati ilionekana kwamba mambo yote yamepotea, Mungu akainua rafiki kwa ajili yake. Staupitz akafungua Neno la Mungu kwa akili wa Luther na akamwomba kutojitazama mwenyewe na kutazama kwa Yesu. “Badala ya kujitesa mwenyewe kwa ajili ya zambi zako, ujiweke wewe mwenyewe katika mikono ya Mwokozi. Umutumaini, katika haki ya maisha yake, malipo ya kifo chake...Mwana wa Mungu alikuwa mtu kukupatia uhakikisho wa toleo ya kimungu. ... Umpende yeye aliyekupenda mbele.” Maneno yake yakafanya mvuto mkubwa kwa ajili ya Luther. Amani ikakuja kwa roho yake iliyataabika. TSHM 53.5
Alipotakaswa kuwa padri, Luther akaitwa kwa cheo cha mwalimu katika chuo kikuu (universite) cha Wittenberg. Akaanza kufundisha juu ya Zaburi, Injili, na kwa barua kwa makundi ya wasikilizi waliopendezwa. Staupitz, mkubwa wake akamwomba kupanda kwa mimbara na kuhubiri. Lakini Luther akajisikia kwamba hastahili kusema kwa watu katika jina la Kristo. Ilikuwa tu baada ya juhudi ya wakati mrefu ndipo alikubali maombi ya rafiki zake. Alikuwa na uwezo mkubwa katika Maandiko, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Kwa wazi uwezo ambao alifundisha nao ukweli ukasadikisha ufahamu wao, na nguvu yake ikagusa mioyo yao. TSHM 54.1
Luther alikuwa akingali mtoto wa kweli wa Kanisa la Roma, hakuwa na wazo kwamba atakuwa kitu kingine cho chote. Akaongozwa kuzuru Roma, aliendelea safari yake kwa miguu, kukaa katika nyumba za watawa njiani. Akajazwa na ajabu hali nzuri na ya damani ambayo alishuhudia. Watawa (moines) walikaa katika vyumba vizuri, wakajivika wao wenyewe katika mavazi ya bei kali, na kujifurahisha kwa meza ya damani sana. Mafikara ya Luther yalianza kuhangaika. TSHM 54.2
Mwishowe akaona kwa mbali mji wa vilima saba. Akaanguka mwenyewe chini udongoni, kupaaza sauti: “Roma mtakatifu, nakusalimu!” Akazuru makanisa akasikiliza hadizi za ajabu zilizokaririwa na mapadri na watawa, na kufanya ibada zote zilizohitajiwa. Po pote, mambo yakamushangaza --uovu miongoni mwa waongozi, ubishi usiofaa kwa maaskofu. Akachukizwa na (unajisi) wao hata wakati wa misa. Akakutana upotevu, usharati. “Hakuna mtu anaweza kuwazia,” akaandika, “zambi gani na matendo maovu sana yako yakitendeka katika Roma. ... Watu huzoea kusema, ` Kama kunakuwa na jehanumu, Roma inajengwa juu yake.’” TSHM 54.3