Tangu Sasa Hata Milele

37/257

Ukweli juu ya ngazi ya Pilato

Kuachiwa kuliahidiwa na Papa kwa wote watakaopanda juu ya magoti yao “Ngazi ya Pilato,” waliozania kuwa ilichukuliwa kwa mwujiza toka Yerusalema hata Roma. Luther siku moja alikuwa akipanda ngazi hizi wakati sauti kama radi ilionekana kusema, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Waroma 1:17. Akaruka kwa upesi kwa magoti yake kwa haya na hofu kuu. Tangu wakati ule akaona kwa wazi kuliko mbele neno la uongo la kutumaini kazi za binadamu kwa ajili ya wokovu. Akageuza uso wake kwa Roma. Tangu wakati ule mutengano ukakomaa kuwa hata akakata uhusiano wote na kanisa la Roma. TSHM 54.4

Baada ya kurudi kwake kutoka Roma, Luther akapokea cheo cha mwalimu (docteur) wa mambo ya Mungu. Sasa alikuwa na uhuru wa kujitoa wakfu mwenyewe kwa Maandiko ambayo aliyapenda. Akaweka naziri (ya ibada ya Mungu) kuhubiri kwa uaminifu Neno la Mungu, si mafundisho ya waPapa. Hakuwa tena mtawa tu, bali mjumbe aliyeruhusiwa wa Biblia, aliyeitwa kama mchungaji (pasteur) kwa kulisha kundi la Mungu lillokuwa na njaa na kiu ya ukweli. Akatangaza kwa bidii kwamba Wakristo hawapaswe kupokea mafundisho mengine isipokuwa yale ambayo yanayojengwa juu ya mamlaka ya Maandiko matakatifu. TSHM 55.1

Makundi yenye bidii yakapenda sana maneno yake. Habari ya furaha ya upendo wa Mwokozi, hakikisho la msamaha na amani katika damu ya kafara yake ikafurahisha mioyo yao. Huko Wittenberg nuru iliwashwa, ambayo nyali yake iongezeke kungaa zaidi kwa mwisho wa wakati. TSHM 55.2

Lakini kati ya ukweli na uongo kunakuwa vita. Mwokozi wetu Mwenyewe alitangaza: “Musifikiri ya kama nimekuja kuleta salama duniani, sikuja kuleta salama lakini upanga.” Matayo 10:34. Akasema Luther, miaka michache baada ya kufunguliwa kwa Matengenezo: “Mungu ... ananisukuma mbele ... nataka kuishi katika utulivu; lakini nimetupwa katikati ya makelele na mapinduzi makuu.” TSHM 55.3