Tangu Sasa Hata Milele
7 / LUTHER, MTU KWA WAKATI WAKE
Wakwanza miongoni mwa wale walioitwa kuongoza kanisa kutoka gizani mwa mafundisho ya Kanisa la Roma kwa nuru ya imani safi zaidi kukasimama Martin Luther. Hakuogopa kitu chochote bali Mungu, na kukubali msingi wowote kwa ajili ya imani bali Maandiko matakatifu. Luther alikuwa mtu anayefaa kwa wakati wake. TSHM 52.1
Miaka ya kwanza ya Luther ilitumiwa katika nyumba masikini ya mlimaji wa Ujeremani. Baba yake alimukusudia kuwa mwana sheria (mwombezi), lakini Mungu akakusudia kumufanya kuwa mwenye mjengaji katika hekalu kubwa ambalo lilikuwa likiinuka pole pole katika karne nyingi. Taabu, kukatazwa, na maongozi magumu yalikuwa ni masomo ambamo Hekima lsiyo na mwisho ilimtayarisha Luther kwa ajili ya kazi ya maisha yake. TSHM 52.2
Baba wa Luther alikuwa mtu wa akili ya kutenda. Akili yake safi ikamwongoza kutazama utaratibu wa utawa na mashaka. Hakupendezwa wakati Luther, bila ukubali wake, akuingia katika nyumba ya watawa (monastere). Ilichunkua miaka miwili ili baba apatane na mtoto wake, na hata hivyo maoni yake yakibaki yale yale. TSHM 52.3
Wazazi wa Luther wakajitahidi kulea watoto wao katika kumjua Mungu. Bidii zao zilikuwa za haki na kuvumilia kutayarisha watoto wao kwa maisha ya mafaa. Nyakati zingine walitumia ukali sana, lakini Mtengenezaji mwenyewe aliona katika maongozi yao mengi ya kukubali kuliko ya kuhukumu. TSHM 52.4
Katika masomo Luther alitendewa kwa ukali na hata mapigano. Akiteswa na njaa mara kwa mara. Mawazo ya giza, na juu ya mambo ya ibada ya sanamu ya dini iliodumu wakati ule ikamuogopesha. Akilala usiku na moyo wa huzuni, katika hofu ya daima kwa kufikiria Mungu kama sultani mkali, zaidi kuliko Baba mwema wa mbinguni. TSHM 52.5
Wakati alipoingia kwa chuo kikubwa (universite) cha Erfurt, matazamio yake yalikuwa mazuri sana kuliko katika miaka yake ya kwanza. Wazazi wake, kwa akili walioipata kwa njia ya matumizi mazuri ya pesa na bidii, waliweza kumusaidia kwa mahitaji yote. Na rafiki zake wenye akili sana wakapunguza matokeo ya giza ya mafundisho yake ya kwanza. Kwa mivuto ya kufaa, akili yake ikaendelea upesi. Matumizi ya bidii upesi ikamutia katika cheo kikuu miongoni mwa wenzake. TSHM 52.6
Luther hakukosa kuanza kila siku na maombi, moyo wake kila mara ukipumuamaombi ya uongozi. “Kuomba vizuri, “akisema kila mara, “ni nusu bora ya kujifunza.” TSHM 52.7
Siku moja katika chumba cha vitabu (librairie) cha chuo kikubwa akavumbua Biblia ya Kilatini (Latin), kitabu ambacho hakukiona kamwe. Alikuwa akisikia sehemu za Injili na Nyaraka (Barua), ambazo alizania kuwa Biblia kamili. Sasa, kwa mara ya kwanza, akatazama, juu ya Neno la Mungu kamili. Kwa hofu na kushangaa akageuza kurasa takatifu na akasoma yeye mwenyewe maneno ya uzima, kusimama kidogo kwa mshangao, “O”, kama Mungu angenipa kitabu cha namna hii kwangu mwenyewe!” Malaika walikuwa kando yake. Mishale ya nuru kutoka kwa Mungu yakafunua hazina za kweli kwa ufahamu wake. Hakikisho kubwa la hali yake kuwa mwenye zambi likamushika kuliko zamani. TSHM 53.1