Tangu Sasa Hata Milele

34/257

Kusalitiwa kwa Njia ya Upatanishi

Waongozi wa Papa mwishowe wakatumia njia ya upatanisho. Mapatano likafanya ambalo kwalo likasaliti wa Bohemia katika utawala wa Roma. Watu wa Bohemia wakataja sharti inne kwa ajili ya amani kati yao na Roma: (1) uhuru wa kuhubiri Biblia; (2) haki ya kanisa lote katika mambo mawili hayo ya mkate na divai katika ushirika na matumizi ya lugha ya kienyeji katika ibada ya Mungu; (3) Kutenga waongozi wa dini la kikristo kwa kazi zote za kidunia na mamlaka; na, (4) wakati wa kosa, hukumu ya baraza za serkali juu ya mapadri na wasiokuwa mapadri iwe sawa sawa. Hukumu za Papa zikakubali kwamba mambo mane yale yakubaliwe, “lakini haki ya kuyaeleza ... inapaswa kuwa kwa baraza--katika maneno mengine, kwa Papa na kwa mfalme.” Roma ikashinda kwa unafiki na madanganyo mambo ambayo kwa njia ya vita alishindwa. Kukubalia Roma uwezo wa kutafsiri maandishi ya wafuasi wa Huss, kama juu ya Biblia, iliweza kupotosha maana kwa kupendeza makusudi yake. TSHM 50.4

Hesabu kubwa ya watu katika Bohemia, kuona kwamba jambo lile lilisaliti uhuru wao, hawakuweza kukubali mapatano. Kutopatana kukaumka, na kuletaugomvi kati yao wenyewe. Procopius mwenye cheo akashindwa, na uhuru wa watu wa Bohemia ukakoma. TSHM 50.5

Tena majeshi ya waaskari ya kigeni yakashambulia Bohemia, na wale waliodumu kuwa waaminifu kwa injili wakawa katika hatari kwa mateso ya damu. Kwani walisimama imara. Wakakazwa kutafuta kimbilio katika mapango, wakaendelea kukusanyika kusoma Neno la Mungu na kujiunga katika ibada yake. Kwa njia ya wajumbe kwa siri wakatuma kwa inchi mbali mbali wakajifunza “kwamba katikati ya milima ya Alps (safu ya milima mirefu) kulikuwa kanisa la zamani, la kudumu juu ya misingi ya Maandiko, na kukataa maovu ya ibada ya sanamu ya Roma.” Kwa furaha kubwa, uhusiano wa kuandikiana ukawa kati yao na Wakristo wa Waendense furaha kubwa, (Vaudois). TSHM 51.1

Msimamo imara wa injili, watu wa Bohemia wakangoja usiku kucha wa mateso yao, katika saa ya giza kuu hata wakageuza macho yao kwa upeo kama watu wanaokesha hata asubui. TSHM 51.2